Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
0712461976 au 0764302956
ASERNAL usiku huu wametupwa nje ya ligi yamabingwa barani Ulaya baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 mechi ya marudiano na mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Bayern Munich, uwanja wa Allianz Arena nchini Ujerumani.
Mechi ya kwanza wakiwa nyumbani kwao Emirates, Asernal walilala kwa mabao 2-0, hivyo matokeo ya leo yanawafanya watolewe kwa wastani wa mabao 3-1.
Msimu uliopita, Asernal walifungwa mabao 3-1 na walipoenda Allianz Arena walishinda 2-0, lakini msimu huu wa UEFA umekuwa majanga baada ya kutoka sare usiku huu.
Bayern walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza dakika ya 55 kupitia kwa kiungo wake, Bastian Schweinsteiger aliyepewa pasi na winga hatari wa klabu hiyo, Mfaransa Frank Ribery.
Ilibaki kidogo Asernal watolewa kwa wastani wa mabao 3-0, lakini alikuwa ni Lukas Podolski katika dakika ya 57 aliyesawazisha bao hilo.
Mambo yalienda kombo zaidi kwa washika bunduki baada ya mwamuzi kuwazawadia penati wenyeji, lakini bahati ikawa kwao baada ya Thomas Muller kukosa penati hiyo dakika ya 90.
Nao AC Milan wametolewa katika michuano hiyo kufuatia kipigo `kitakatifu` cha mabao 4-1 kutoka kwa Atletico Madrid, hivyo kutupwa nje kwa mabao 5-2 kwani walifungwa kwao bao 1-0.
Matokeo ya mechi za leo yako hivi;
International: Champions League Final Stages
Finished
|
Atletico Madrid
| 4-1 |
AC Milan
| (2-1) | ||||||
Finished
|
Bayern Munich
| 1-1 |
Arsenal
|



Kimoja tu: Bastian Schweinsteiger akishangilia baada ya kuifungia Bayern bao la kuongoza

Schweinsteiger akifunga bao lake

Amekosa: Lukas Fabianski akiokoa penati ya Thomas Muller dakika za lala salama

Uaminifu : Bayern wakiwashukuru mashabiki wao baada ya sare ya leo usiku
0 comments:
Post a Comment