YANGA KUIVAA ALTAY SK !!
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara na vinara wa ligi hiyo timu ya Young Africans itashuka dimbani siku ya jumatano kucheza mchezo wa pili wa kirafiki wa kujipima nguvu na timu ya Altay S.K iliyopo Ligi Daraja la Pli nchini Uturuki.
Kikosi cha Young Africans kimeendelea na mazoezi leo asubuhi na jioni katika viwanja vya hoteli ya Sueno Beach Side kujiandaa na mchezo huo wa siku ya jumatao ambao ni sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya klabu Bingwa barani Afrika.
Kaimu kocha mkuu Charles Mkwasa amesema anashukuru vijana wake wote wanaendelea vizuri katika kambi ya mafunzo, hakuna mchezaji ambaye amekosa mazoezi hata siku moja na hali ya hewa inaruhusu kabisa kufanya mazoezi hivyo vijana wanaitumia ipasavyo nafasi hiyo.
Akiongelea mchezo wa keshokutwa Mkwasa amesema anawaandaa vijana kuendelea kufanya vizuri katika mchezo huona ataendelea kutoa nafasi kwa kila mchezaji aliyekuja nchini Uturuki apate nafasi ya kucheza kwani kupata nafasi ya kucheza michezo ya kirafiki huku ni njia ya kuwakomaza na kuweza kujiamani katika michezo ya kimataifa.
Kesho timu ya Young Africans itafanya mazoezi mara moja tu asubuhi kujiandaa na mchezo huo wa jumatano dhidi ya timu ya Altay SK ambayo pia inajiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Daraja Pili nchini Uturuki.
Mara baada ya mchezo huo wa jumatano Young Africans itakamlisha ziara yake ya mafunzo wiki ijayo kwa kucheza na timu ya Simurq Zaqatala FC ya nchini Azberbaijan iliyopo katika Ligi Kuu ya nchi hiyo na msimu uliopita ikiwa imekamata nafasi ya nne kwenye msimamo wa Azerbaijan Premier League.
0 comments:
Post a Comment