Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itacheza
mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia (Brave Warriors) ikiwa ni sehemu ya
maandalizi ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika (AFCON)
zitakazochezwa mwakani nchini Morocco.
Stars na Brave Warriors zitacheza mechi hiyo Machi
5 mwaka huu jijini Windhoek, Namibia. Mechi hiyo ipo katika kalenda ya mechi za
kirafiki za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Makubaliano ya kucheza mechi hiyo yamefikiwa
kutokana na mazungumzo kati ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Jamal Malinzi na Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Namibia (NFA), John
Muinjo.
Benchi la Ufundi la Brave Warriors linaongozwa na
kocha mzawa Ricardo Mannetti, na mechi hiyo itachezwa ama Uwanja wa Sam Nujoma
au Uwanja wa Uhuru jijini Windhoek.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium
Lager inafundishwa na kocha Kim Poulsen kutoka Denmark na inatarajia kuanza
kucheza mechi za mchujo za AFCON Septemba mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment