Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Tel: 0712461976 au 0764302956
MAAFANDE
wa jeshi la kujenga Taifa wa mkoani Pwani, Ruvu Shooting, wamemsainisha
mkataba wa miezi sita kocha, Tom Alex Olaba ili kurithi mikoba ya
kocha aliyetimkia Yanga, Charles Boniface Mkwasa `Masta`.
Afisa
habari wa klabu hiyo, Masau Bwire amesema Olaba ameshafika Mabatini
jioni ya leo na kila kitu kimemalizika baina ya pande mbili.
“Tunafurahi
kutangaza kuwa tumempata mrithi wa Mkwasa. Olaba ni mwalimu mzuri na
tuna uhakika atatuongoza vizuri mzunguko wa pili”. Alisema Masau.
Olaba
ambaye amewahi kuifundisha Mtibwa Sugar ataanza kazi rasmi kesho
kukinoa kikosi cha Ruvu Shooting kuelekea mzunguko wa pili wa ligi kuu
soka Tanzania bara unaotarajia kuanza kutimu vumbi januari 25 mwaka huu.
Kwa
upande wake Olaba alisema amefurahi kurudi ligi kuu Tanzania bara kwa
mara nyingine, lakini hawezi kuzungumza lolote mpaka atakapoongea na
wachezaji wake hapo kesho mazoezini.
“Nimechoka
sana ndugu yangu, ujue nimetoka safarini. Hata hivyo kwasasa siwezi
kuzungumza lolote mpakaa nikikutana na kuongea na wachezaji wangu.
Kikubwa nimefurahi kurudi katika changamoto ya ligi ya Tanzania”,
Alisema Olaba.
0 comments:
Post a Comment