Tuesday, January 14, 2014

Mbunge  wa  viti maalum mkoa wa  Iringa  Ritta Kabati wa  pili kushoto akiwa na madiwani na  viongozi  wengine wa CCM Iringa mjini  leo wa  pili  kushoto  kwake  ni mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza ,katibu  wa CCM wilaya Hassan Mtenga,Meya Aman Mwamwindi na  kushoto wa kwanza  diwani wa kata ya Kitwiru Ally Mbata



Wananchi  wakiwa katika mkutano  huo  leo



Wananchi  Iringa mjini  wakiwa  wamejipanga kwa  maswali katika mkutano wa CCM Iringa mjini leo


Diwani  wa kata ya Mtwivila Bw  Victor Mushi  akijibu  maswali ya  wapiga kura  wake  katika mkutano huo  wa CCM
 
Iringa mjini  leo
……………………………………………………………….
Na  Francis Godwin Blog Iringa
 CHAMA  cha mapinduzi (CCM) wilaya ya  Iringa  mjini kimeanza  kufufua matumaini  ya  wananchi  wa  jimbo la Iringa  mjini  juu ya  kero  zinazowakabili  kwa  kuwaweka kitimoto madiwani  wake  katika mkutano wa hadhara kwa  kumtaka  kila mwananchi kumhoji  diwani  wake kama anatosha ama  hatoshi  kuendelea  kuwaongoza.
Huku  wananchi  wa  jimbo  hilo la Iringa  mjini  wakikitaka  chama hicho kusaidia  kukinusuru  chama  na  kura  za chuki  kutokana na shirika la ugavi  wa umeme nchini (TANESCO)  kuendelea  kupandisha  gharama  za  umeme.
Wakihoji  katika mkutano  huo  wa  hadhara   uliofanyika katika uwanja  wa Mwembetogwa  leo  ,wananchi  hao  walisema  kuwa  ili CCM jimbo  hilo na Tanzania kwa ujumla kiweze  kushinda katika uchaguzi  mkuu wa mwaka 2015  na ule wa  serikali za mitaa utakaofanyika mapema mwaka  huu ni lazima gharama  za umeme ishuke
Kwani  walisema  kuwa  hatua ya  TANESCO  kuendelea  kuongeza  bei ya  umeme  ni  kuongeza  ugumu  wa maisha  kwa  watanzania na kuwa ushindi  wa CCM  utatokana na utetezi  wa chama katika  kuwaondolea  mzigo  wa bei ya umeme watanzania.
Mbali  ya  hilo pia  wananchi  wa  kata ya Kihesa walimbana  diwani  wao Bw  Mussa Wanguvu  kutokana na hatua ya  kushindwa  kupigania  wananchi ambao  wanatakiwa  kuvunja  nyumba  zao ambazo  zimejengwa katika eneo la  Semtema Majengo  mapya eneo ambalo halitakiwi  kisheria
Diwani  Wanguvu  akijibu  swali  hilo alisema  kuwa eneo  hilo  lilizuiwa baada ya kufanyika kwa mkutano wa hadhara  hasa  wale  ambao  wamejenga katika mlima na wapo hatarini  kuangukiwa na mawe  ila baadhi ya maeneo ambayo  si  rasmi  ni waliachiwa .
Kwa  upande  wao  wananchi  wa kata ya Mtwivila  walimtaka diwani  wao Bw  Victor Mushi  kueleza  ni  lini atatekeleza ahadi yake  ya zahanati na ubovu  wa barabara katika  eneo la Mkimbizi pamoja .
Kwa  upande  wake diwani Mushi  kuhusu  suala  la ujenzi  wa  kituo cha afya  alisema  kuwa ahadi hiyo haikuwa ya kwake  ila  ilikuwa katika ilani  ya  CCM  japo alisema ujenzi  wa  mradi huo  upo mbioni  baada ya  kumaliza miradi ya zamani utaanza mradi huo  wa ujenzi  wa  kituo cha afya.
Kuhusu  barabara  alisema  kuwa kata  hiyo  wamejitahidi  kutengeneza  mifereji na zaidi ya Tsh  bilioni 1.8  zitatengeneza  barabara  ya lami  kutoka Mtwivila  kwenda Mkwawa  na tayari  zoezi hilo linaendelea.
Katika  hatua  nyingine  Mushi  alipinga  madai ya  wananachi  kuwa  uongozi  wa Halmashauri  ya Manispaa ya  Iringa  umekuwa  ukifanya usafi  katika mji  kutokana na kuwepo kwa ugeni ama  vikao  kuwa jambo  hilo  si kweli na kuwa linafanyika kulingana na bajeti  na ufinyu  wake.
Katibu  wa CCM wilaya ya  Iringa mjini Hassan  Mtenga  alisema  kuwa  lengo la  kuwaweka  kitimoto madiwani ni  kutaka  kukata mzizi wa  fitina na kuanzisha  utaratibu mpya  wa CCM kutekeleza  ilani yake pamoja na kupokea  kero za  wananchi.
Hata  hivyo  alisema  utaratibu  huo  utaendelea kama njia ya  kukiwezesha chama hicho  kuweza  kupata  ushindi  wa  kimbunga  katika chaguzi  zijazo.
Mstahiki  meya  wa Manispaa ya  Iringa Aman Mwamwindi  akijibu kero mbali mbali akianza na Hospital ya  wilaya ya Iringa  mjini alisema kuwa  Hospital  hiyo  imeendelea  kutoa huduma .
Huku  ujenzi  wa barabara  za lami katika mji  huo kupitia pesa za benk ya Dunia  alisema barabara  itajengwa kuanzia  Samora ,Hospital ya Frelimo , Itamba na maeneo mengine ya mji .
Kuhusu  suala la usafi  alisema  kuwa moja kati ya sababu  zilizopelekea mji wa Iringa  kutoshika nafasi ya kwanza ni kutokana na hadhi ya makaburi na ndio  sababu makaburi ya makanyangio  kuanza  kuzungushiwa  uzio ili  siku moja  Manispaa ya  Iringa  iweze  kushika nafasi ya kwanza .
Alisema kuwa ni vema  suala la maendeleo  ya mji wa Iringa lisifanyike kwa itikadi  za  vyama na badala  yake  kufanyika  kutokana na mazingira yaliyopo .
Kuhusu  suala la Stendi ambalo limeendelea  kuleta lugha mbali mbali kutoka serikalini na viongozi  wa kisiasa alisema  kuwa hashangai na kauli  za  upotoshwaji juu ya ujenzi wa stendi hiyo ya kisasa ya mkoa itakayogharimu  zaidi ya Tsh bilioni 4  fedha  kutoka benki ya  dunia .
Alisema  kuwa mchakato  wa ujenzi  wa  stendi  hiyo umeshirikisha  wadau  wote  nyeti hadi  mshauri  wa mambo ya kimazingira  kimataifa  na tayari ameifanya kazi  hiyo na  kutoa maelekezo  yake ya kitaalam ambapo ameruhusu ujenzi huo.
Alisema inapojengwa  stendi hiyo  kutoka ukingo wa mto ni mita zaidi ya 700 wakati sheria ya ujenzi ya Rufiji na Iruwasa ni mita kati ya 50 na 60 hivyo stendi  hiyo ipo mbali zaidi  kuliko sheria.
Alisema  kuwa fedha  za ujenzi  wa stendi hiyo hata kama Halmashauri ingekusanya isingeweza kupata  fedha  hizo ambazo hata kama ingekusanya kwa miaka  zaidi ya 3 bila kupata .
Alisema  kuwa  wanaotumia maendeleo  kwa ajili ya kutafuta umaarufu katika  siasa ni kutowatendea haki  wananchi ambao  unawatumikia na kuwa suala la uongo halikubariki katika dini  zote .
Hata  hivyo  Mwamwindi  alisema jitihada mbali mbali  zinazofanywa na serikali ya  CCM  katika manispaa ya  Iringa ni kutaka  kuiwezesha  Halmashauri  hiyo kuja kuwa jiji kama   ilivyo Mbeya, Mwanza na Arusha .
Hivyo  alisema tayari  jitihada mbali mbali  za  kuwezesha mji wa Iringa kuwa jiji na tayari  wamepeleka mradi  wa maji Nduli mradi  ambao wakati wa kuwekeana  saini  mbunge  wa jimbo la Iringa mjini alipata  kushiriki .
“Tumepeleka  barabara  kutoka Tumaini  kwenda  Kigonzile KM 6   tumepeleka mabati kwa ajili ya choo mgongo pamoja na kuweka  vituo katika eneo la Kigonzile  ili kupeleka huduma  hiyo kwa  wananchi … kwa  hiyo ndugu zangu mheshimiwa Mushi amezungumzia  barabara  ya kutoka Mkimbizi hadi bima  kiasi cha mabilioni ya  fedha  ambazo binafsi sijapata  kusaini fedha nyingi kiasi  hicho ….sasa  tumeanzisha mkakati wa kugawa  viwanja na kupasua  njia na ninasema kuwa ujenzi  wa stendi upo pale pale na suala  hili lipo kwa waziri mkuu ambaye  ndie mwenye  TAMISEMI”

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video