Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
Tel: 0712461976 au 0764302956
MABINGWA
watetezi mara mbili mfululizo wa kombe la Mapinduzi, Azam fc wameanza
vyema michuano hiyo baada ya kuifunga Spice Stars mabao 2-0 katika
mchezo wa Kundi C jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mabao
ya Azam fc yamefungwa katika dakika ya 71 kupitia kwa Mshambuliaji
Mganda, Brian Umony kufuatia kuwatoka mabeki wa Spice na kupiga mpira
uliomshinda mlinda mlango, Mohamed Silima.
Pasi ya bao hilo litoka kwa kiungo mahiri wa Azam fc Salum Abubakar ‘Sure Bo”.
Bao
la pili lilifungwana na Himid dakika ya 86 kwa shuti kali, baada ya
kuuwahi mpira uliokuwa unaelekea mikononi mwa kipa Silima kufuatia shuti
la Salum Abubakar.
Afisa habari wa Azam fc ameuambia mtandao huu kuwa mchezo ulikuwa mgumu sana kwani wapinzani wao wameonekana kuwa imara.
“Tumeanza
vizuri kwa ushindi, lakini inaonekana michuano ya mwaka huu ni migumu
sana. Spice wameonesha upinzani mkubwa sana kwetu, lakini hatuwezi
kusema lolote kwani ni mapema sana”. Alisema Jafar.
Jafar
aliongeza kuwa kocha wao Mcameroon, Joseph Marius Omog anakisuka kikosi
chao, hivyo makosa yanayotokea yatafanyiwa marekebisho na kuhakikisha
wanatwaa ubingwa wao.
Aidha,
Jafar kwa niaba ya viongozi wa Azam fc amewapongeza vijana wao kwa
kujituma na kupata ushindi ambao haukuwa rahisi kabisa.
Kwa ushindi huo, Azam inaongoza Kundi C kwa pointi zake tatu, na kubaki au kushuka itategemea na matokeo ya mchezo wa pili usiku wa leo leo Uwanja wa Amaan kati ya Ashanti United ya Dar es Salaam na Tusker FC ya Kenya.
Kwa ushindi huo, Azam inaongoza Kundi C kwa pointi zake tatu, na kubaki au kushuka itategemea na matokeo ya mchezo wa pili usiku wa leo leo Uwanja wa Amaan kati ya Ashanti United ya Dar es Salaam na Tusker FC ya Kenya.
Kueleka katika mchezo huo, wauza mitumba wa Ilala wamesema wapo tayari kuwamaliza wakenya.
Marijani
rajab, afisa habari wa Ashanti ameuambia mtandao huu kuwa kocha mkuu wa
kikosi chao, Abdalaah Kibaden Mputa amewapanga vijana wake kutokana na
uzoefu wake katika michuano mikubwa barani Afrika.
Katika mchezo mwingine wa Kundi A, Uwanja wa Gombani, Pemba, URA ya Uganda imetoka sare ya 2-2 na Chuoni ya Zanzibar.
Mabao ya URA yamefungwa na Owen Kasuule dakika ya 44 na 57, wakati ya Chuoni yalifungwa na Shaaban Moke dakika ya 21 na Mwinyi Mngwali dakika ya 45
Mabao ya URA yamefungwa na Owen Kasuule dakika ya 44 na 57, wakati ya Chuoni yalifungwa na Shaaban Moke dakika ya 21 na Mwinyi Mngwali dakika ya 45
0 comments:
Post a Comment