Tel: 0712461976 au 0764302956
KLABU ya Yanga ya jijini Dar es salaam imeitafuna KMKM kutoka Visiwani Zanzibar mabao 3-2 kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa jioni ya leo uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Yanga waliingia uwanjani na kujitahidi kutafuta matokeo ya ushindi na hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji wake hatari, Jerryson John Tegete akimalizia pasi ya kichwa ilipigwa na mshambuliaji raia wa Burundi, Didier Kavumbagu `Kavu`.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kucheza kwa kasi na katika dakika ya 48 beki nguli wa klabu hiyo na nahodha, Nadir Haroub `Canavaro` aliandika bao la pili akiunganisha mpira mrefu wa kurushwa wa beki kisiki, Raia wa Rwanda, Mbuyu Twite.
KMKM walifanikiwa kuchomoa bao la kwanza katika dakika ya 69 kupitia kwa Hajji Simba aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Ame Khamis.
KMKM walifanikiwa kuchomoa bao la kwanza katika dakika ya 69 kupitia kwa Hajji Simba aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Ame Khamis.
Wakati Yanga wakidhani ni bao la kufutia machozi, Ally Ahmed `Shiboli` aliyewahi kucheza Simba SC aliisawazishia bao la pili klabu yake katika dakika ya 72.
Dakika sita baadaye (dakika ya 78), Kiungo Khamis Thabit aliandika bao la tatu na la ushindi kwa klabu yake ya Yanga kwa shuti kali akiwa eneo la miguu 18 ya mtu mzima.
Baada ya mchezo wa leo, KMKM kesho wana kibarua kingine cha dakika 90 kukabiliana na klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa mechi za kirafiki.
Ili kuhakikisha anawasoma wapinzani wake kabla ya mchezo wa kuhitimisha kampeni ya `Nani Mtani Jembe?’ utakaowakutanisha na Yanga, kocha mkuu wa Simba, Mcroatia Zdravko Logarusic alikuwa uwanjani leo hii.
Hiyo ni mara ya kwanza kuwaona wapinzani wake (Simba Sc) wakicheza kabla ya kumenyana nao desemba 21 mwaka huu.
Logarusic amerithi mikoba ya kocha Abdallah Kibadeni aliyetimuliwa na Simba baada ya kumaliza katika nafasi ya nne mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Kibadeni kwa sasa ni kocha wa wauza mitumba wa Ilala, klabu ya Ashanti United inayohaha kutafuta nguvu za mzunguko wa pili wa ligi kuu.
0 comments:
Post a Comment