Saturday, December 14, 2013


Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
Tel: 0712461976 au 0764302956
MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Yanga ya Dar es salaam leo hii i ndani ya uwanja wa Taifa inashuka ugani kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya maafande wa KMKM kutoka visiwani Zanzibar ikiwa ni maandalizi ya mechi yao ya kuhitimisha kampeni ya Nani Mtani Jembe, desemba 21 mwaka huu.
Mechi hiyo itakuwa maalum kwa benchi la ufundi la klabu hiyo chini ya  kocha mkuu, Ernie Brandts akisaidia na Fredy Minziro kuwapima vijana wao kabla ya kula sahani moja na Mnyama Simba.
Kuelekea katika mechi hiyo, maandalizi yote yamekalika na baada ya mechi ya leo, nao Wekundu wa Msimbasi Simba watashuka dimbani kesho kuwakabili KMKM katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.
yangaSimba na Yanga zinajiandaa na pambano la `KAMPENI YA NANI MTANI JEMBE`ambalo  ni zawadi ya kufungia mwaka kwa mashabiki na kila timu imetia sahihi makubaliano kwamba itachezesha kikosi cha kwanza ili kuwapa mashabiki burudani ya uhakika.”
 Hivi karibuni, Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema  kuwa mechi hii ni maalum kwa ajili ya kuhitimisha kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo imeendeshwa kwa zaidi ya miezi miwili ikiwapa fursa mashabiki wa timu hizi kuchangia timu zao kila wanapoburudika na bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Kilimanjaro Premium Lager   ilitenga kiasi cha shilingi milioni 100 zinazoshindaniwa na Simba na Yanga kupitia mashabiki wake na tarehe 21 Desemba ndio utakuwa mwisho wa kampeni ya Nani Mtani Jembe ambapo baada ya mechi  fedha hizo zitagawanywa kwa kila timu kulingana na matokeo ya kura za mashabiki na klabu zitajiamulia namna ya kutumia fedha hizo.
IMG_4530
Kuelekea katika pamano hilo la mechi hiyo, kocha msaidizi wa Yanga, Fredy Ferlix Minziro, `Katalaiya Majeshi, Baba Isaya` amesema vijana wote wapo salama, morali yao ni kubwa sana kuelekea kuwakabili Simba Sc.
“Ni nafasi nyingine kwa vijana wetu kuonesha uwezo wao mkubwa mbele ya Simba baada ya sare ya 3-3 katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara”. Alisema Minziro.
Minziro alitamba kuwa Simba walimshukuru sana Mungu baada ya sare ya 3-3, lakini mtihani mwingine mgumu kwao  umekaribia ukizingatia wao Yanga ni  bora kuliko wao.
“Kutoka nyuma kwa mabao 3-0 na kusawazisha na hatimaye kupata sare ya 3-3  ilikuwa bahati yao na walimshukuru sana Mungu. Desemba 21 wanaingia uwanjani wakiwa na mchecheto mkubwa kwani wanafahamu wazi kazi yetu ilivyo bora”. Alijigamba Minziro.
Kuelekea mechi hiyo, Yanga wataingia uwanjani wakiwa na wachezaji wapya, Juma Kaseja na Hassan Diliunga ambao wamethibitishwa kupewa mikataba na klabu hiyo.
Kwa upande wa Simba, wao wataingia wakiwa na wachezaji kadhaa wapya wakiwemo makipa Ivo Mapunda, Yaw Berko, kiungo  Awadh Issa Juma kutoka Mtibwa, beki kutoka Gor Mahia ya Kenya, Donald Mosoti Omwanwa na wengine.
Pia wataingia uwanjani wakiwa na makocha wapya, Mcroatia, Zdravko Logarusic akisaidiwa na msaidizi wake ambaye ni kiungo wa zamani wa klabu hiyo na aliyekuwa kocha wa timu ya Simba B, Seleman Matola `Veron`.
Kwa mazingira hayo, benchi la Ufundi la Simba SC litahitaji kutafuta ushindi ili kujenga imani kwa mashabiki wao wenye machungu ya kuzidiwa na watani zao wa jadi, klabu ya Yanga, wakati Yanga wataingia na sura zilezile za benchi la ufundi.
yanga simbaMbilingembilinge za Nani Mtani Jembe? kuhitimishwa Desemba 21, Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam 

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video