Na Fatma Salum
Wazazi
na Walezi wamesisitizwa kuwapeleka watoto wenye umri wa Miezi sita hadi
miaka Mitano kupata matone ya vitamin A yanayotolewa kwenye vituo vya
Huduma za afya Kote nchini.
Msisitizo
huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe toka Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Vincent Assey wakati wa Mkutano na
waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.
Dkt.
Assey alisema kuwa zoezi la utoaji matone ya vitamin A kwa watoto
linalofayika mara mbili kwa mwaka kila mwezi juni na disemba huenda
sanjari na utoaji wa dawa za Minyoo kwa watoto wenye umri wa mwaka mmoja
hadi miaka mitano.
Dkt. Assey alisisitiza kuwa matone hayo ni Muhimu kwa watoto kwani yanasaidia katika ukuaji,maendelezo ya afya na uhai wa mtoto.
“Ni
muhimu kwa wazazi na walezi wafahamu kuwa, vyakula tunavyokula
havikidhi mahitaji ya vitamin A mwilini kwa Mtoto, kwani mahitaji yao ni
makubwa hivyo watoto hawana budi kupewa matone ya vitamin A mara mbili
kila mwaka ili kukidi mahitaji hayo” Alisema Dkt. Assey.
Naye
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sayansi ya Chakula na Lishe kutoka Taasisi a
Chakula na Lishe (TFNC) Dkt. Elifatio Towo alisema kuwa watoto walio
katika umri wa Miaka Mitano wanapaswa kupewa vyakula vyenye Vitami A kwa
Wingi kama Mboga za Majani ,Matunda, Dagaa, mafuta ya Mawese na Maini
ili kuwaongezea vitamin hiyo isiyotengenezwa na Mwili hivyo ni lazima
itokane na vyakula.
Aidha
Dkt. Towo aliongeza kuwa madhara yatokanayo na upungufu wa vitamin A
mwilini ni pamoja na kutokuona vizuri kwenye Mwanga hafifu, upofu,
maradhi ya Mara kwa Mara na Vifo vya watoto, hivyo ili kupambana na
tatizo hilo yapaswa kuzigatia unyonyeshaji sahihi wa watoto,ulaji wa
vyakula vyenye virutubisho na watoto kupatiwa matone ya vitamin A.
Takwimu za kitaifa juu ya demografia na afya ya jamii (Demographic and Health Survey)za
mwaka 2010 zinaonesha kuwa hapa nchini upugufu wa Vitamin A unaathiri
asilimia 33 ya watoto walio chini ya Umri wa miaka 5 na Asilimia 37 ya
wanawake walio katika Umri wa Kuzaa.
0 comments:
Post a Comment