Sunday, December 15, 2013


IMG_4865ZAIDI ya watu elfu kumi wa kata ya olasiti na mateves  waliokuwa wakikabilwa na ukosefu wa maji safi na salama  kwa kipindi cha miaka 50 wameondokana na tatizo  hilo kufuatia shirika la world vision kufadhili  mradi wa matanki  manne yenye gharama ya shilingi milioni 8,.
Aidha wananchi hao hapo awali kabla ya kupata mradi huo walikuwa wanalazimika kutembea umbali wa kilometa tano kutafuta maji hayo huku akina mama  kupigwa na waume zao na watoto wa kike wakinusurika kubakwa .
Akizungumza na gazeti hili katibu wa mradi wa mangole uliopo katika kata hiyo Asha Shabani alisema kuwa mradi huo ulianza kazi rasmi
mwaka jana na kwamba umesaidia kwa kiasi kikubwa sana kupunguza hadhi hiyo ambayo imewakabili kwa muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi.
Alieleza kuwa hapo awali wananchi wa eneo hilo walikuwa wakifuata maji jeshini ambapo pana umbali mrefu na wanapoishi hali ambayo ilikuwa ikiwaletea madhara katika familia zao kwani walikuwa wanachelewa kurudi majumbani hivyo kusababisha ugomvi ndani ya ndoa.
Alisema kuwa kupitia tatizo hilo lililokwakumba kwa muda mrefu pia watoto wao walikuwa wanashawishika sana kwani baadhi ya vijana
walikuwa wanatumia muda huo kwa ajili ya kuwarubuni kimapenzi hali ambayo ilikuwa ikihatarisha sana maisha ya watoto wao.
Nae mwenyekiti wa mradi huo Kelvin Marriale alisema kuwa mradi huo umesaidia sana kwa kiwango kikubwa kwani hata mifugo wanaofugwa maeneo hayo nayo imeongezeka kwa kuwa robo tatu ya idadi ya mifugo wanakunywa maji yanayotokana na mradi huo tofauti na hapo awali ambapo hata mifugo walikuwa hawaongezeki.
Hata hivyo Marriale aliitaka serikali kuongeza nguvu zaidi ili maji yaweze kusambaa zaidi na hatimaya yaweze kukidhi mahitaji halisi ya
binadamu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video