Na Baraka Mpenja
TIMU
ya Taifa ya Tanzania bara, The Kilimanjaro Stars imefanikiwa kutinga
hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika
mashariki na kati, CECAFA baada ya kuitafuna Burundi bao 1-0 alasiri ya
leo.
Shukurani
kubwa zimwendee nyota wa Tanzania anayekipiga klabu ya TP Mazembe,
Mbwana Samatta aliyefunga bao hilo pekee katika dakika ya 7 akiunganisha
kwa ufundi mkubwa krosi iliyochongwa na Mtanzania mwenzake anayekipiga
klabu ya Tp Mazembe, Thomas Ulimwengu.
Stars
imecheza soka zuri na kupata nafasi nyingi za kufunga, lakini umahiri
wa kipa wa Burundi, Arakaze Arthur amewaokoa Warundi kwani aliokoa
bunduki nyingi langoni mwake.
Kwa
Matokeo ya mchezo wa leo, Kili Stars imemaliza mechi za makundi
ikijikusanyia pointi 7 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Zambia, kisha
kuifunga Somalia 1-0 mechi za awali, na leo hii kuibuka na ushindi wa
bao 1-0 dhidi ya Burundi.
Nani
atakuwa kinara wa kundi B, matokeo ya mchezo unaoendelea sasa baina ya
Zambia na Somalia utaamua ambapo mpaka sasa ni mapumziko na Zambia wako
mbele kwa mabao 2-0.
Kama
Zambia itaibuka na ushindi mkubwa leo hii basi itaongoza kundi B, na
tafsiri yake ni kuwa Kilimanjaro Stars itakumbana na Uganda katika
mchezo wa robo fainali.
Iwapo
Kili stars itakutana na Uganda, itakuwa na hamu ya kulipa kisasi kwani
walilala 3-0 katika mchezo wa nusu fainali wa michuano iliyopita mjini
Kampala, Khamis Kiiza na Emmanuel Okwi wakiwemo ndani kwani mwaka huu
pia wamejumuishwa kwenye kikosi cha Uganda The Cranes.
kama Stars itaongoza Kundi B, itakutana na Timu ya Taifa ya Rwanda, `Amavubi` .
Tanzania
Bara; Ivo Mapunda, Himid Mao, Erasto Nyoni, Said Morad, Kevin Yondan,
Frank Domayo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Amri Kiemba/Haroun Chanongo
dk77, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na Mrisho Ngassa/Ramadhani
Singano ‘Messi’ dk81.
Burundi; Arakaza Arthur, Hakizimana Hassan/Abdulrazack Fiston dk81, Hererimana Rashid, Hakizimana Issa, Nsabiyumva Frederic, Nduwimana Jean, Ndikumana Yussuf, Duhayinavyi Gael/Mussa Mosi, Nduwarugira Christophe, Habonimana Celestin na Hussein Shaaban/Ndarusanze Claude.
Burundi; Arakaza Arthur, Hakizimana Hassan/Abdulrazack Fiston dk81, Hererimana Rashid, Hakizimana Issa, Nsabiyumva Frederic, Nduwimana Jean, Ndikumana Yussuf, Duhayinavyi Gael/Mussa Mosi, Nduwarugira Christophe, Habonimana Celestin na Hussein Shaaban/Ndarusanze Claude.
0 comments:
Post a Comment