Na KIBADA Kibada Katavi
Wanaume
Mkoani Katavi wamepewa changamoto kutoa taarifa kwa jeshi la polisi
wanapofanyiwa vitendo vya unyanyasaji na wake zao.
Changamoto
hiyo ilitoewa hivi na Mkuu wa Kitengo Jeshi la polisi Mkoani Katavi
kupitia kitengo cha dawati la jinsia na unyanyasaji wa watoto sodoka
vijinia Sodoka katika maazimisho ya siku kumi na sita ya kupinga
unyanyasaji wa watoto na wanawake pia hata wanaume wananyanyaswa na wake
zao majumbani na kukaa kimya bila kutoa taarifa kwa jeshi la polisi
hivyo hakuna taarifa sahihi kuhusu hilo.
Kutokana na changamoto hiyo
jamii inatakiwa kuelewa na kufichua maovu ya unyanyasaji wanayofanyiwa
watoto katika Mkoa wa Katavi.Amevitaja baadhi ya vitendo hivyo wanavyofanyiwa watoto na wanawake walio wengi majumbani kuwa ni kupigwa ,kuchomwa moto kunyimwa chakula.
Vitendo vingine ni pamoja na ubakaji ili kwa hali hiyo wasikae kimywa watoe taarifa polisi watasaidiwa na wataweza kufichuliwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
wiki ya unyanayasaji kinjisia ambapo wameazishwa kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo.
Bi
Sodoka akiongea kwa nyakati tofauti katika wadi ya wazazi,wadi, ya
wanaume na wadi ya watoto katika kauli zake amewashauri wazazi
kuhakikisha watoto wanapofanyiwa vitendo vya unyanyasaji kama kubakwa
wapelekwe polisi ndani ya masaa 72 kabla ya kwenda Hospitali ili sheria
iweze kuchukua mkondo wake wao polisi watatoa utaratibu wa kibali cha
kwenda Hospitali kutibiwa na mhusika atachukuliwa hatua lakini kama
hawatatoa ushirikiano hawatafahamu kinachoendelea.
Akizungumzia
mahusiano ya Jeshi la polisi na jamii alisema wao ni sehemu ya jamii
hivyo hawana budi kushirikiana kwa ukaribu na jamii wanayoishi nayo ili
kudumisha amani na usalama katika jamii hiyo.
Kwa
upande wake mmoja wa wauguzi aliyepokea zawadi kutoka kitengo cha dawati
la jinsia Bi Lucy Baruti alifurahishwa na kitendo cha jeshi la polisi
kuwathamini na kuja kuwaona wagonjwa kwa kuwaletea zawadi za sabuni,
biskuti na mafuta ambavyo vitasaidia kwa njia moja au nyingine
kuwafariji wagonjwa.
0 comments:
Post a Comment