Wakazi wa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wanakusudia kuanzisha Kituo cha Redio ya kijamii kwa ajili ya kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii na shughuli nyingine za maendeleo katika eneo hilo ili kuongeza kipato kwa wananchi wake na taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Mandalizi ya Harambee ya uanzishaji wa Redio Rungwe FM Bw. Christopher Andendekisye wakati akizungumza waandishi wa habari .
Alisema kuwa Mkoa wa Mbeya na husasani Wilaya ya Rungwe inavyo vivutio vingi ambavyo kwa sababu ya kukosa chombo cha mawasiliano kama vile Redio vimekuwa havifahamiki kwa wananchi wengi wan je ya Wilaya hiyo na hivyo kuikosesha Serikali mapato ambayo yangetokana na sekta ya utalii.
Bw. Andendekisye alisema kuwa kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili Wilaya Rungwe, Uongozi wa Christian na Gospel Ministry umeamua kuanzisha mchakato wa usajili Redio inayoitwa Rungwe FM, ikiwa ni Redio ya kijamii kwa ajili ya kuhamasisha shughuli mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kisiasa ndani ya Wilaya ya Rungwe.
Alisema Redio hii tayari ipo katika orodha ya redio zilizoomba usajili wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania [TCRA], imesajiliwa mwezi septemba mwaka 2013.
Kufuatia hali hiyo Bw. Andendekisye aliwaomba wananchi na wakazi wa Wilaya ya Rungwe kusaidia upatikanaji wa shilingi milioni 170 zinahitaji kukamilisha ununuzi wa vifaa vitakavyosaidia uanzishwaji wa redio hiyo mapema.
Aliongeza kuwa hadi hivi sasa wameshapata ahadi ya shilingi milioni 92 na kuongeza kuwa ili kumalisha kiwango chote wanatarajia kufanya harambee mwezi Machi 2014 katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Bw. Andendekisye alisema kuwa kwa mwananchi atakayehitaji kuwachangia anaweza kutuma fedha zake kupitia akaunti 038201043087 Tukuyu Christian Fellowship –NBC Bank
0 comments:
Post a Comment