Monday, December 16, 2013


Dk. Ibrahim Msengi
Dk. Ibrahim Msengi
Serikali  imeiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro kuacha mara moja kugawa bure miche ya kahawa ya vikonyo inayotolewa na Taasisi ya Utafiti wa Kahawa nchini (TaCRI) kwa kuwa wakulima wa zao hilo wanaweza wasiuthamini mpango huo kwa kutogharamia.
.Mkuu wa Wilaya hiyo,  Dk. Ibrahim Msengi alitoa agizo hilo juzi wakati alipowatembelea wakulima akiwemo mkulima bora wa kahawa, Didas Malya, mkazi wa Kibosho ambaye ameshinda nafasi ya kwanza ya mkulima wa mfano katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
Akiwa katika Kijiji cha Manushi-Sinde, Dk. Msengi alisema baadhi ya wakulima wa zao hilo mkoani hapa wanadaiwa kuitumia vibaya fursa hiyo ya kugawiwa bure miche hiyo na badala yake wamekuwa hawaitunzi na kusababisha zaidi ya asilimia 50 kuwa katika hali mbaya na mingine kufa.
“Japokuwa wana nia njema ya kugawa miche hii bure kwa wakulima, ipo haja ya kutafuta utaratibu mwingine, ikiwamo wakulima kuchangia gharama… kutoa bure kunasababisha asiithamini na hii inasababisha lengo kutotimia, ” alisema Dk. Msengi.
Alisema kwa mujibu wa taarifa alizonazo, asilimia kubwa ya miche iliyogawanywa kwa wakulima ipo katika hali mbaya jambo linalochangiwa na tabia ya baadhi ya watu kutothamini vitu vya bure.
Kwa upande wake mtafiti na msambazaji wa teknolojia ya uzalishaji mbegu bora wa TaCRI,Jeremia Magesa amezitaka halmashauri zinazolima kahawa kuiga mfano wa Moshi kuwekeza katika kilimo cha zao hilo.
Alisema mfano ulioonyeshwa na Moshi Vijijini wa kuigwa kwani fedha zinazotokana na zao hilo zitasaidia kuiongezea mapato halmashauri hiyo.
 Kaimu Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya hiyo, Chikira Mcharo, alisema katika kampeni hiyo,  wilaya imeanzisha na kusimamia mashamba 52 ya mfano wa kilimo cha kahawa bora kwa wakulima vijijini.
Kwa upande wake Mkulima Malya  amewataka wakulima wenzake kutokata tamaa na changamoto mbali mbali ikiwamo ya kushuka kwa bei ya kahawa na kusisitiza umuhimu wa kuzalisha iliyo bora
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video