Sunday, December 15, 2013

cb4a0-1375766_581274061909694_1850204431_n---CopyNa Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
Tel: 0712461976 au 0764302956
Tanzania Prisons `Wajelajela` wameshaanza maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania bara unaotarijia kuanza kutimua vumbi januari 25 mwaka huu.
Katibu mkuu wa klabu hiyo, Inspekta Sadick Jumbe amesema wameamua kuingia kwenye mawindo mapema ili kumpa muda wa kutosha kocha wao mpya David Mwamwaja.
“Tupo katika maandalizi ndugu yangu. Mzunguko wa pili utakuwa mzuri kwasababu tuna mechi nyingi za nyumbani. Tutatumia kila mchezo wa nyumbani kusaka pointi tatu muhimu ili kuendelea kuwepo ligi kuu”. Alisema Jumbe.
Jumbe alisema mzunguko wa kwanza ulikuwa mbaya kwao na ndipo uongozi wa klabu hiyo ukaamua kumfungashia virago kocha wake, Jumanne Chale aliyeonekana kutokuwa na msaada kwao.
“Mwamwaja aliongoza mechi za mwisho za mzunguko wa kwanza. Timu ilionekana kubadilika sana hasa katika mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Rhino Rangers kule Tabora licha ya kutoa suluhu, lakini timu ilikuwa na kiwango kizuri”. Aliongeza Jumbe.
Inspekta huyo aliendelea kusisitiza kuwa, Prisons haitakuwa daraja la kuvuna pointi kwa timu za ligi kuu licha ya sasa kuwa nafasi ya pili kutoka mkiani.
Jumbe alisema msimu uliopita walipambana mpaka dakika ya mwisho kukwepa kushuka daraja na msimu huu watakaza uzi zaidi kutafuta matokeo mazuri kama ilivyo kwa ndugu zao wa Mbeya City FC ambao walimaliza mzunguko wa kwanza bili kufungwa mechi yoyote.
“Sisi tuko imara sana ndugu yangu. Utaamini maneno yangu ligi ikianza. Kikubwa mashabiki wa Mbeya watuunge mkono. Waache ubaguzi kwani Mbeya City Fc na Tanzania Prisons ni ndugu”. Alisema Jumbe.
Tangu Mbeya City FC ipande ligi kuu imejizolea mashabiki wengi ndani na nje ya jiji la Mbeya wakati Prisons inaonekana kutokukubalika sana”. 

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video