Thursday, December 5, 2013


Jennifa Chiwute
Mwakilishi wa Mitandao ya Kijamii nchini (CCT), Jennifa Chiwute

Watoto yatima nchini  wako hatarini  kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ilikinganishwa na kundi la wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.
Akizungumza jana katika  mdahalo  ulioandaliwa na mtandao wa kupinga ukatili wa kijinsia (MKUKI) ulioratibiwa na  Shirika la Kupinga Ukatili wa Kijinsia Tanzania (AFNET)Kanda ya Kati uliofanyika mjini hapa, Mwakilishi wa Mitandao ya Kijamii nchini (CCT), Jennifa Chiwute, alisema  taarifa ya  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa mwaka 2009 kuhusiana na vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini,  imeonyesha kundi hilo la watoto yatima liko kwenye hatari zaidi ya kufanyiwa vitendo hivyo kwa kuwa wengi wao hawana ulinzi kutoka kwa mtu yeyote.
Akiwasilisha mada kuhusiana na mpango wa kukomesha vitendo hivyo, Chiwute,  alisema taarifa hiyo ilionyesha kuwa asilimia 30 ya wasichana na asilimia 14.3 ya wavulana,  waliwahi kutendewa kitendo kimoja cha ukatili wa kijinsia kabla ya kufikisha umri wa miaka 18 huku asilimia 60 ya wasichana walilazimishwa kujamiina.
Alibainisha  pia inaonyesha kuwa wasichana hao walilazimishwa kujamiiana na ndugu,  jirani, marafiki na watu wasiowafahamu wenye umri mkubwa.
“Waathirika wenyewe wanafanyiwa kwenye maeneo ya nyumbani kwa mtu, shuleni au njiani wakati wa kwenda au wa kurudi shuleni,” alisema Chiwute.
Alisema vitendo hivyo ni pamoja  na ukatili wa kipigo, ukeketaji, kingono na kiakili.
Alionya kuwa iwapo vyombo vya dola havitachukua hatua za kisheria kwa wanaotenda vitendo hivyo, hali itazidi kuwa mbaya zaidi kwa siku zijazo.
“Vyombo vya serikali vimeshindwa kusimamia kwa dhati utekelezaji wa sheria zinazolinda haki za wanawake, watoto na watu wenye ulemavu kwa sababu ya rushwa,”alisema Chiwute.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa  AFNET Tanzania,  Sarah Mwaga, alisema ni wajibu wa wadau wote na watetezi wa haki za binadamu kuungana kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vina madhara makubwa kwa watendewa.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Dawati la Jinsia Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, Hamida Hiki, alisema kuwa jeshi hilo linakabiliwa na changamoto ya jamii kuwa na mfumo dume ambao ndiyo chanzo cha vitendo vya ukatili ambavyo vinasababisha wimbi la watoto wa mazingira hatarishi mitaani.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video