Na Miza Othman Maelezo-Zanzibar
Serikali,
Jamii na Taasisi zisizokuwa za kiserikali zimeombwa kushughulikia suala
la udhalilishaji wa kijinsia kwa vitendo ili kuhakikisha kwamba suala
la ukatili wa kijinsia linaondoka kabisa Visiwani hapa.
Hayo
yameelezwa leo huko Ea- crotanal na Mkurugenzi wa Maendeleo Wanawake na
Watoto Rahma Ai Khamiss ikiwa ni maadhimisho ya siku ya 16 za
wanaharakati wakupiga vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Amesema
kwamba Wizara imetayarisha mpango wa utekelezaji wa kisekta zidi ya
udhalilishaji wa kijinsia ambao unalengo la kuweka mtandao wa sekta na
kuunganisha jitihata za kupiga vita vitendo vya udhalilishaji wa
kijinsia.
Aidh
Mkurugenzi Rahma Ali amesema kwani hivi sasa kumeshapitshwa sheria ya
motto zidi ya uzalilishaji iliyopitishwa mwenzi wa Machi 2011
uliozingatia upatikanaji wa haki, fursa na ulinzi wa motto wakiwemo
wakikie kupitia taasisi husika na jamii kwa ujumla.
Wizara
kwa kushirikiana na taasisi husika imefanyia mapitio sheria ya mahakama
ya kadhi ya mwaka 1985 ili kubaini mapungufu yake katika kutoa haki kwa
waathirika wa vitendo vya udhalilishaji wakijinsia, alisema
Mkurugenzi Rahma Ali.
Nae
Msaidizi Afisa Watoto Mohammed Jabir Makame amesema endapo mtoto
amefanyiwa ukatili wa kijinsia hupata athari ya ulemavu wa viungovya
kawaida na uzazi,kushindwa kusoma vizuri,kuongezeka kwa mimba zisizo
tarajiwa na kuongezeka kwa virusi vinavyosababisha ukimwi.
Hata
hivyo amesema ni vyema wazazi kuwa na wawasiwasi wa mara kwa mara na
kuchukuwa jitihada za makusudi kwa kufuatilia nyenendo za watoto wao
wakati wanapo kwaenda Skuli, Chuoni na hata wanapokwenda kucheza na
wenzao.
Kongamano
hilo Dlilijumuishavitengo mbali mbali wakiwemo Askari, Dactarina
Maafisa kutoka Mkoa wa Kaskazini Unguja,Kusini Unguja na Mkoa wa Mjini.
Ujumbe wa mwaka huu ni Amani ya Duniani huanzia Nyumbani tupigane na vitendo vya utumiaji wa nguvu zidi ya wanawake na watoto.
IMETOLEWA NAIDARAYA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
0 comments:
Post a Comment