Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
Tel: 0712461976 au 0764302956
HATIMAYE Makundi ya hatua ya 16 bora ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya imetolewa mchana huu, huku Manchester City ya England ikitumbukia mdomoni mwa miamba ya soka nchini Hispania, FC Barcelona.
Nao washika bunduki wa London, klabu ya Asernal imepangwa na mabingwa watetezi, wekundu wa kusini mwa Ujerumani, Bayern Munich.
Didier Drogba anarudi tena kuivaa klabu yake ya Zamani ya Chelsea akiwa na mabingwa wa Uturuki, Galatasaray.
Mashetani Wekundu angalau wameonekana kubebwa na droo hii baada ya kupangiwa timu ya Olympiacos ya nchini Ugiriki.
Makunndi yamepangwa ifuatavyo;
Manchester City v Barcelona
Olympiacos v Manchester United
AC Milan v Atletico Madrid
Bayer Leverkusen v Paris St Germain
Galatasaray v Chelsea
FC Schalke v Real Madrid
Zenit v Borussia Dortmund
Bayern Munich v Arsenal


Droo imefanyika eneo la Nyoni, na imeendeshwa na katibu mkuu wa UEFA, Gianni Infantino, Mkurugenzi wa mashindano wa UEFA , Giorgio Marchetti na balozi , Luis Figo.
Washindi wa makundi wataanzia ugenini katika mechi za kwanza ambazo zitafanyika kati ya tarehe 18/19, 25/26 mwezi wa pili mwakani huku Mechi za marudiano zitakuwa kati ya 11/12, 18/19 mwezi wa tatu mwakani.


0 comments:
Post a Comment