Tamasha kubwa la Ujasiriamali lililofikia tamati jana jioni katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza lilitawaliwa na elimu pamoja na burudani kali kutoka kwa wasanii Fid Q, H-Baba, Young Killer na Jitta Man. Kwa upande wa injili, burudani hizo ziliongozwa na Martha Mwaipaja na Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji. Walimu wa ujasiriamali nchini, Eric Shigongo na James Mwang’amba wakiwa sambamba na Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Mhe. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ walitoa elimu ya ujasiriamali kwa wakazi wa Mwanza na kuwaacha wakiwa wameiva kwenye masuala hayo.
(PICHA: CHANDE ABALLAH NA DENIS MTIMA / GPL, MWANZA)
0 comments:
Post a Comment