WILAYA YA RUNGWE – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 26.12.2013 MAJIRA YA SAA 20:10HRS HUKO ENEO LA KATUMBA, KATA YA KATUMBA, TARAFA YA TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA, BARABARA YA MBEYA/TUKUYU. GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU AMANI S/O ABILIA, MIAKA 22, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA KATUMBA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MAKANDANA – TUKUYU. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI HASA KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KWENYE MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
[B.N.MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment