WILAYA YA MOMBA – UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA .
MNAMO TAREHE 16.12.2013 MAJIRA YA SAA 19:45HRS HUKO KATIKA ENEO LA SOGEA – MAKAMBINI, KATA YA TUNDUMA, TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA, ALPHONCE S/O MWANJELA, MIAKA 36, KYUSA, MFANYABIASHARA YA KUBADILISHA FEDHA, MKAZI WA SOGEA – MAKAMBINI ALIVAMIWA NA KUNDI LA WATU WANNE WASIOFAHAMIKA KISHA KUMKATA MAPANGA KICHWANI NA KUMJERUHI KWA KUMPIGA RISASI MGUU WA KULIA KWA KUTUMIA BUNDUKI IDHANIWAYO KUWA S/GUN NA KUMPORA PESA TASLIMU TSHS 5,200,000/=, USD 2,300, RAND 10,000 NA ZAMBIA KWACHA 2,000,000. WATUHUMIWA HAO WALIMVAMIA MHANGA AKIWA UMBALI WA MITA 50 TOKA NYUMBANI KWAKE WAKATI ANATOKA KATIKA SHUGHULI ZAKE ZA KUBADILISHA FEDHA MPAKANI TUNDUMA. MHANGA AMELAZWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI. MSAKO MKALI UNAENDELEA DHIDI YA WAHUSIKA WA TUKIO HILI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA YA KUBADILISHA FEDHA WAJIUNGE PAMOJA WAFUNGUE DUKA LA KUBADILISHA FEDHA AMBALO LITAKUWA LIMESAJILIWA ILI ULINZI UWE RAHISI ILI KUONDOA SUALA LA KUTEMBEA NA FEDHA KIHOLELA NA KUFANYA WIZI/UPORAJI NA UNYANG’ANYI KUWA RAHISI. PIA ANATOA WITO KWA WALE WANATAKA KUBADILISHA FEDHA WAENDE KATIKA TAASISI RASMI ZA KUBADILISHA FEDHA KWA USALAMA ZAIDI KWANI UWEZEKANO WA KATAPELIWA NI MDOGO. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA YA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE
WILAYA YA CHUNYA – TAARIFA YA KIFO.
MNAMO TAREHE 16.12.2013 MAJIRA YA SAA 16:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA CHOKAA, KIJIJI CHA KIBAONI, KATA YA CHOKAA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA, EZEKIA D/O AZIGETI, MIAKA 10, MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI SHULE YA MSINGI CHOKAA, ALIKUFA MAJI WAKATI AKIOGELEA NA WATOTO WENZAKE KWENYE MTO CHUNYA. CHANZO NI BAADA YA MAREHEMU KUZIDIWA NA MAJI WAKATI AKIOGELEA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO WAO HASA KIPINDI HIKI CHA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA KWA KUTOWARUHUSU KWENDA KUOGA KATIKA MITO/MABWAWA/MATIBWI YA MAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUFUNIKA/KUFUKIA NA KUZIBA MASHIMO NA VISIMA VILIVYOWAZI ILI KUEPUKA MATUKIO YA WATOTO WADOGO KUFA MAJI.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA SILAHA [GOBOLE].
MNAMO TAREHE 15.12.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MANDA “B”, KIJIJI NA KATA YA GUA, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA CHUNYA, MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA KWA USHIRIKIANO NA WAHIFADHI WA HIFADHI YA NGWALA WALIMKAMATA OCTAVIAN S/O ISMAIL, MIAKA 38, MBUNGU AKIWA NA SILAHA GOBOLE MOJA KINYUME NA SHERIA. MTUHUMIWA NI MUWINDAJI HARAMU, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOMILIKI SILAHA KINYUME NA SHERIA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
[BARAKAEL MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment