WILAYA YA MBARALI – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 1.12.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MPAKANI BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE KATA YA IGAWA TARAFA YA RUJEWA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. MTU MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA KIUME MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 37-40 ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUCHOMWA KISU KICHWANI NA SHINGONI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA KANDO YA BARABARA HIYO. CHANZO CHA MAUAJI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA MBARALI KWA UCHUNGUZI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA NAIBU KAMISHNA WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA YA MAHALI ALIPO MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA MOMBA – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 13.12.2013 MAJIRA YA SAA 14:30HRS HUKO MAENEO YA MTAA WA MWAKA BARABARA YA TUNDUMA/SUMBAWANGA KATA YA TUNDUMA, TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. GARI T. 904 BXV AINA YA M/CANTER LIKIENDESHWA NA DEREVA MAAMZEE S/O MOHAMED, MIAKA 21, MNYIHA, MKAZI WA MTAA WA MWAKA – TUNDUMA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA KIKE, UMRI KATI YA MIAKA 25-30 NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA KWA AJILI YA UCHUNGUZI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA NAIBU KAMISHNA WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA MWISHO WA MWAKA.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI – DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment