MKurugenzi
wa Kampuni ya Blue Sky, Richard Signeski (kulia), akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani), katika ukumbi Club ya Escape, Mikocheni jijini Dar es Salaam Desemba
3, 2013 kuhusu Kampuni ya Status Communications ya nchini kushirikiana
na Kampuni ya Usambazaji wa filamu ya kimarekani ya Blue Sky Media ili
kuweza kuuza filamu kwenye mitandao. Kushoto ni Mwakilishi wa Status
Communication, Monalisa Shayo.
PICHA HABARI NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM
Kampuni
ya Status Communications leo imetangaza ushirikiano na kampuni ya
usambazaji wa filamu ya kimarekani Blue Sky Media ili kuwawezesha kuuza
filamu kwenye mitandao ya ITunes, Microsoft, You Tube, RAIN na mitandao
mingine ya kimataifa.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Blue Sky, Richard Signeski
alisema ushirikiano huu utawafanya watengeneza filamu kutoka Afrika
Mashaaiki na kati kuweza kuuza filamu moja kwa moja kwenye mitandao
mikubwa ya usambaji dunia nzima.
‘’Lengo
la ushirikiano huu ni kuwapa watengeneza filamu kutoka Afrika mashariki
na kati kuweza kuuza filamu zao moja kwa moja kwa watazamaji dunia
nzima’’ alisema Signeski.
Mwakilishi
wa Status Communications, Monalisa Shayo alisema ushirikiano wao na
Blue Sky ni moja ya tu ya ushirikano na makampuni ya kimataifa wanaotaka
kuingia katika soko la Afrika Mashariki.
‘’Mwaka
2013 umekuwa mwaka muhimu kwa Status Communications kwani tumeweza
kuingia mikataba na makampuni mbalimbali ili kuweza kuingia soko la
Afrika Mashariki’’ alisema Monalisa.
‘’Mwanzoni
mwa mwaka huu tumeingia mikataba na makampuni kama Media Zone
Authority ya Abu Dhabi (twofour54) pamoja na Qatar’s Media Group
International pamoja na Visual Unity ya Abu Dhabi ili kuwawakilisha
kwenye masoko yao kwenye miji kama ya Prague’ alisisitiza Monalisa wa
Status Communications.
‘’Fursa hii ni muhimu kwa watengeneza filamu wa Afrika Mashariki kuuza filamu kwenye masoko tofauti duniani’’ alisema Monalisa.
Akielezea
sababu za kuja nchini, Signeski alisema alichokigundua hapa nchini ni
kuwa watengeneza filamu wengi wanahofia kuwekeza fedha nyingi kwenye
utengenezaji wa filamu zao kwani wanahofia uchache wamasoko ya kuuza
filamu zao.
‘’Hivyo nawaomba watengeneza filamu mjitokeze kwa wingi ili muweze kuuza filamu dunia nzima kwa urahisi’’ alimaliza Signeski.
0 comments:
Post a Comment