Monday, December 16, 2013


SIMBA imepangwa kufungua pazia la michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kucheza na AFC Leopards ya Kenya Januari Mosi wakati Yanga wakishuka dimbani siku inayofuata kuikabili Tusker FC.
Msemaji wa Kamati ya Michuano ya Kombe la Mapinduzi, Farouk Karim alisema, pambano la Simba na Leopards litafanyika kwenye Uwanja wa Amani saa 2 usiku na litatanguliwa na mechi kati ya wenyeji KMKM na KCC ya Uganda litakalopigwa saa 10 jioni kwenye uwanja huohuo.
195Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic akiwa na vijana wake kwenye moja ya mazoezi uwanja wa Kinesi jijini Dar es salaam. Picha na Maktaba
Katika michuano iliyopita Simba waliishia nusu fainali baada ya kuondolewa na Azam FC kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya mechi kumalizika kwa sare ya 2-2 hata baada ya kuongezwa dakika 30.
Nao mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga yenyewe haikushikiri michuano iliyopita kutokana na kuwa katika ziara ya mechi za kirafiki nchini Uturuki lakini mwaka huu imethibitisha ushiriki wao.
Yanga itashuka uwanjani Januari 2 kuivaa Tusker ya Kenya mchezo utakaochezwa saa 2 usiku kwenye Uwanja wa Amani na utatanguliwa na mchezo kati ya Azam na Kombaini ya Unguja utakaochezwa saa 10 jioni.
615_340_AFC-Leopards-playersFC Leopards
Pia kutakuwa na mechi nyingine Januri 2 zitakazofanyika kwenye Uwanja wa Gombani Pemba kati ya URA ya Uganda itakayoikabili Chuoni majira ya saa 8 mchana na baadaye itafuatiwa na mchezo kati ya Mbeya City dhidi ya Kombaini ya Pemba utakaofanyiak saa 10 jioni.
Farouk alisema robo fainali ya michuano hiyo itafanyika Januari 8, wakati nusu fainali itafanyika Januri 10 na fainali Januari 13.
Alisema, mechi zote za hatua ya makundi na robo fainali zitafanyika kwenye viwanja wa Gombani Pemba na Amani Unguja, wakati nusu fainali na fainali zitapigwa kwenye Uwanja wa Amani.
CHANZO: MWANASPOTI

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video