Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sporstmail
Tel: o712461976 au 0764302956
MSHAMBULIAJI hatari wa mabingwa watetezi wa ligi kuu soka nchini England, klabu ya Manchester United, Robin van Persie atakaa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na matatizo ya mguu.
Mholanzi huyo aliumia mguu akipiga mpira wa kona uliozaa bao wakati wa mechi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya jumanne ya wiki hii dhidi ya Shakhtar Donetsk ambapo Man United walishinda bao 1-0 na sasa atakaa nje ya dimba mpaka mwaka mpya.
Habari hizo zimemchefua na kumvuruga kabisa kocha wa Man United, David Moyes ambaye anapigana kuepukana na kipigo cha tatu mfululizo ndani ya miaka 11 kwani Jumapili anajiandaa kuvaana na Aston Villa.
Muda mwingi nje ya dimba: Robin van Persie alionekana akiwa amebaba mapochopocho jana maeneo ya Alderley Edge akielekea masikani yake
Hapa home tu: Van Persie akirudi katika gari lake baada ya kununua chakula cha mchana katika kijiji kidogo cha Cheshire
Nje: Mholanzi, van Persie atakaa nje ya uwanja kwa wiki nne kufuatia kupata majeruhi ya mguu
Van Persie atakaso mechi zifuatazo wakati huu
Aston Villa (A), Dec 15, Premier League
Stoke (A), Dec 18, kombe la ligi
West Ham (H), Dec 21, Ligi kuu
Hull (A), Dec 26, Ligi kuu
Norwich (A), Dec 28, Ligi kuu
Tottenham (H), Jan 1, Ligi kuu
Swansea (H), Jan 5, kombe la FA
Swansea (H), Jan 11, Ligi kuu
Moyes alisema : ‘Robin Van Persie atakaa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja`.
‘Aliumia wakati akipiga mpira wa kona iliyozaa bao.’
Moyes aliongeza: `Ni bahati mbaya sana kwetu kwasababu ukiangalia rekodi yetu tunapokuwa na Wayne Rooney na Robin timu kiukweli infanya vizuri sana na ikumbukwe hatujawa nao kwa muda sasa.
‘Marouane Fellaini naye ana maamivu kidogo ya mgongo`.
‘Michael Carrick hayupo na Robin atakaa nje ya uwanja kwa wiki nne kutokana na matatizo ya mguu. Hilo ni balaa sana kwetu.’
Safari ngumu: Kuna janga lingine kwa David Moyes akijianda kuwafuata Aston Villa keshokutwa jumapili
0 comments:
Post a Comment