Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sporstmail
Tel: 0712461976 au 0764302956
KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers anafikiria kumvika heshima ya unahodha nyota wake Luis Suarez wakati huu ambao nahodha wake Steven Gerrard yuko nje ya uwanja.
Gerrard anatarajia kukosa mechi nne zijazo kutokana na majeruhi ya nyama ya paja- na anatarajiwa kurudi uwanjani katika hatua ya tatu ya kombe la FA.
Hata hivyo, Rogers ana wachezaji wengi wa kucheza katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Tottenham na mechi nyingine, ingawa kumkosa Gerrard ni pigo kwake.
Daniel Agger aliteuliwa kuwa nahodha msaidizi majira ya kiangazi na anaweza kuchukua nafasi hiyo endapo atakuwepo kwenye mchezo wa kesho baada ya kukosa mechi ya wikiendi iliyopita kwa matatizo ya kuumwa ambapo walishinda mabao 4-1 dhidi ya West Ham.
Nahodha?: Luis Suarez (juu) anaweza kupewa unahodha wakati huu ambao nahodha Steven Gerrard huyupo
Wamemkosa: Gerrard (kulia) atakaa nje ya uwanja kwa wiki sita kutokana na majeruhi ya nyama za paja
Lakini Agger amekuwa akisumbuliwa sana na majeruhi msimu huu na sasa Rodgers anafikiria kumpa majukumu Suarez. Mshambuliaji huyo amekuwa na kiwango kizuri sana katika michezo 10 aliyocheza.
Meneja wa Liverpool alionesha nia hiyo jana baada ya kuulizwa nani atakuwa nahodha.
Kama nyota huyo raia wa Uruguay atapewa nafasi hiyo, itamuongezea nguvu zaidi na kupunguza sinema ya yeye kuondoka Anfield majira ya joto mwakani.
Alipoulizwa kama anamfikiria Suarez katika nafasi hiyo muhimu, Rodgers alijibu; `Ndiyo, nafikiria sana- tena kwa asilimia 150″.
Nyota: Suarez (katikati) amekuwa katika kiwango kikubwa akiwa na Liverpool na mpaka sasa amefunga mabao 15 katika michuano ya ligi kuu
Daaah!: Brendan Rodgers (juu) anaamini Suarez anaweza zaidi ya kawaidia kuwa nahodha wa Liverpool
Kiongozi: Suarez (juu) yupo kwenye presha kubwa kuongoza klabu yake wakati huu ambao Gerrard na Daniel Sturridge ni majeruhi
Kuelekea mchezo wa kesho, Lewis Holtby amesisitiza kuwa ni muda mwafaka kwa Tottenham kujipima wenyewe kwa Liverpool.
Mchezo wa kesho endapo Spurs watashinda watafikisha pointi sawa na vijana wa Rodgers.
Holtby, 23, anaamini Spurs wamerudisha morali ya ushindi na kilichobaki ni kudhihirisha hilo hapo kesho kwenye mchezo dhidi ya timu kubwa ya Liverpool.
Kiungo huyo alisema: “Tumerudi katika hali yetu baada ya kipigo kibaya cha 6-0 kutoka kwa Manchester City na nadhani tumejiamini tena na tunaweza kucheza vizuri mbele ya timu nzuri ya Liverpool”.
“Tunatakiwa kucheza mpira wa kushambulia na tunatakiwa kuonesha katika mchezo mkubwa wa kesho, hususani tukiwa nyumbani”.
Aliongeza kuwa ni juu yao kuhimili presha hii kubwa.
Wamejiamini: Lewis Holtby anaamini Tottenham wapo tayari kudhihirisha uwezo wao hapo kesho dhidi ya Liverpool
Wakati huo huo ratiba ya ligi kuu nchini England ni kama ifuatavyo
Leo jumamosi Desemba 14
Manchester City
| - |
Arsenal
| ||||||||
14/12 18:00
|
West Ham
| - |
Sunderland
| |||||||
14/12 18:00
|
Newcastle United
| - |
Southampton
| |||||||
14/12 18:00
|
Everton
| - |
Fulham
| |||||||
14/12 18:00
|
Chelsea
| - |
Crystal Palace
| |||||||
14/12 18:00
|
Cardiff
| - |
West Bromwich Albion
| |||||||
14/12 20:30
|
Hull
| - |
Stoke
|
Kesho Jumapili Desemba 15
England: Premier League
15/12 16:30
|
Aston Villa
| - |
Manchester United
| ||||||
15/12 16:30
|
Norwich
| - |
Swansea
| ||||||
15/12 19:00
|
Tottenham
| - |
Liverpool
|
0 comments:
Post a Comment