THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: [email protected]
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemtumia Salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na
kupitia kwake, kwa mkewe Bi. Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi
wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela
kilichotokea tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.
“Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu”. Ameongeza Rais Kikwete.
“Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu”. Ameongeza Rais Kikwete.
Rais
amemuelezea Mzee Mandela kuwa ni kielelezo cha aina yake kwa wanadamu
kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomuwezesha kuwaunganisha
wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa taifa moja baada ya kipindi kirefu
cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.
“Mandela
ni mfano bora kwa wanadamu wa jinsi binadamu muungwana anavyopaswa
kuwa . Ni wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia kwa jumla kuiga
mfano wake hasa moyo wake wa uzalendo, kujitolea hata maisha yake kwa
ajili yake na wananchi wenzake” .Rais ameongeza kusema, “Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Mandela mahali pema peponi”.
Kufuatia kifo hicho Rais ametangaza siku 3 za maombolezo kuanzia leo tarehe 6 hadi 8 Disemba, 2013.
Aidha, Mheshimiwa Rais ameagiza kuwa katika siku hizo 3 bendera zote zipepee nusu mlingoti.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu,
DAR AS SALAAM.
06 Desemba,2013
0 comments:
Post a Comment