Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi WA Kituo cha Vosa Mission Hochimin Mugarura (kulia) mbuzi mbili(2), kilo 100 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia ikiwa zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa jana na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerekehe sikukuu.
Picha na MAELEZO_ Dar es salaam
Na Kiza Sungura-MAELEZO_Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Dkt Jakaya Mrisho kikwete ametoa jumla ya kilo za mchele 1,200 , lita 220 za mafuta na mbuzi 25 kwa ajili ya zawadi ya sikukuu ya Krismas kwa makundi maalum.
Zawadi hizo zilikabidhiwa jana (leo) na Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bibi Beatrice Fungamo kwa niaba ya Rais Kikwete kwenye sherehe fupi iliyofanyika katika Uwanja wa Mahabusu ya Watoto jijini Dar es salaam.
Alisema kuwa Rais Kikwete ametoa zawadi ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum kama vile yatima, wazee wasiojiweza na watato walioko katika mkinzano na Sheria ili nao waweze kuungana na Watanzania wengine katika kusherekea sikukuu ya Krismas.
Bibi Fungamo alisema kuwa nje ya kutoka zawadi kwa vituo mbalimbali vya Mkoa wa Dar es salaam pia ametoa katika makunndi mengine ya mikoa mingine hapa nchini.
Alisema kuwa kwa upande wa Dar es salaam ametao kwa vituo 11 vinavyosaidia kutoa huduma kwa watoto na wazee wasiojiweza ambazo ni Kituo cha Watoto Ibn Kathir, Tabata, Ilala, Makao ya Watoto Kurasini, Temeke, Makao ya Watoto Yatima Msimbazi, Kituo cha Kwetu Mbagala Girls Home, Kituo cha Yatima Group, na Kituo cha CHAKUWAMA.
Vingine vya mkoani Dar es salaam ni Mahabusu ya Watoto, Makao ya Watoto Yatima Mburahati, Kituo cha Tuwapende Watoto Bunju, Makao ya Wazee wasiojiweza Msimbazi na Vosa Mission Kongowe.
Alisema kuwa kwa vituo vya mikoani na maeneo mengine nje ya Dar es salaam zawadi zao watapatiwa katika maeneo yao .
Bibi Fatuma alivitaja vituo vya nje ya Dar es salaam vilipatiwa zawadi na Rais Kikwete ni Kituo cha Mabaoni Chakeckale Pemba, Kituo cha Werezo cha Unguja, Mahabusu ya Wototo Moshi mkoani Kilimanjaro na Makao ya Wazee wasiojiweza Sukamaela mkoani Singida.
Vingine ni Makao ya wasiojiweza Bukumbi, Misungwi mkoani Mwanza na Makazi ya Wazee wasiojiweza Msufini , Muheza mkoani Tanga.
Alisema kuwa Rais Kikwete ametoa zawadi hizo kwa kutambua kuwa watoto na wazee hao wanapaswa kujumuika na wanajamii wengine katika kusherehekea sikukuu hiyo vema.
Hatua hii ya Rais Kikwete ni sehemu ya utamaduni wake aliojijengea wa kuwakumbuka watu wenye mahitaji mbalimbali .
0 comments:
Post a Comment