Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanyakazi wa TAZARA
………………………………………………………………………
Na Mwandishi, Wetu Mbeya
CHAMA Chama Cha Mapinduzi (CCM),
kimesema kuwa kitamshauri Rais Jakaya Kikwete akutane na mwenzake wa
Zambia Miachael Sata, ili kumaliza matatizo yanayolikabiliwa Shirika la
Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA).
Kutokana na hatua hiyo na
malalamiko ya wafanyakazi CCM imesema kuwa ikiwa Serikali za nchi hizo
zimeshindwa kuliendesha shirika hilo ni vema ikakabidhiwa Serikali ya
China.
Kauli hiyo ameilewa leo mjini hapa
na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana,
alipokuwa akijibu kero zinazowakabiliwa wafnyakazi wa TAZARA upande wa
Tanzania ambapo amesema alisema kuwa shirika hilo limekuwa linakabiliwa
na changmoto kadhaa ikiwemo kushindwa kujiendesha kwa ufanisi.
“Tunajua sasa TAZARA imekuwa
ikikabiliwa na matatizo mengi hivyo ninapenda kukubaliana nanyi
wafanyakazi kuwa shirika hili hivi sasa limekuwa linahujumiwa kwa
makusudi. Haiwezekani mapato yanayopatika kwa kwa kipindi cha miezi
mitatu ni Sh bilioni 7.
“Mishahara ya wafanyakazi ni Sh
bilioni 1 kwa mwezi halafu hawalipwi hadi maandamano na migomo hili si
sawa hata kidogo,” alisema Kinana
Kutokana na hali hiyo Katibu Mkuu huyo wa CCM alisema kuwa atamshauri Jakaya Kikwete aweze kukutana na Rais mwenzake wa Zambia Michael Sata ili kuweza kumaliza changamoto 34 zinazolikabili shirika hilo.
Kutokana na hali hiyo Katibu Mkuu huyo wa CCM alisema kuwa atamshauri Jakaya Kikwete aweze kukutana na Rais mwenzake wa Zambia Michael Sata ili kuweza kumaliza changamoto 34 zinazolikabili shirika hilo.
Reli ya TAZARA ilijengwa mwaka
1975 kama reli ya ukombozi ambayo kwa sasa imekuwa ikitoa huduma ya
usafiishaji wa kizigo na abiri kwa nchi za Tanzania na Zambia
0 comments:
Post a Comment