Saturday, December 14, 2013


steve_nyerere
Mwigizaji Steve Nyerere, ameonyesha masikitiko yake kufuatia kifo cha Rais wa Kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela (Madiba), akieleza kuwa bado alikuwa akihitaji kujifunza kutoka kwake.
Alisema kwamba alijifunza mengi kutoka kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ikiwamo hekima, upendo na kujiamini, lakini alikuwa akihitaji kujifunza kusamehe kutoka kwa marehemu mzee Madiba kwa kuwa ni moja ya sifa zake.
Alifafanua kuwa uasi, chuki, mapambano na migomo ni nguvu ya kushindwa kusamehe ambayo Madiba hakuwa nayo, jambo alilolitaja kulisikitikia kwa kukosa nafasi ya kupata siri hiyo kutoka kwa Madiba.
“Najua alisamehe na sisi hatuna budi kusamehe, lakini kama ningepata bahati ya kuambiwa na mwenyewe alipata wapi ujasiri wa kuwasamehe wote waliomkosea, ningefurahi zaidi. Lakini sina jinsi zaidi ya kumtakia safari njema huko aendako,”alisema Nyerere.
CHANZO: MWANANCHI

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video