Monday, December 16, 2013

mtibwa-640x360Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Tel: 0712461976 au 0764302956
WANA TamTam, Mtibwa Sugar wanaingia kambini leo kuanza kampeni za maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania unaotarajia kuanza kutimua vumbi januari 25 mwaka huu.
Afisa habari wa klabu hiyo, Tobias Kifaru Lugalambwike amesema wapo katika maandalizi ya kuwapokea vijana wao wanaotarajia kuanza kuwasili leo hii tayari kwa kuanza kambi
 “Mzunguko wa kwanza vijana wetu walikosa umakini, walikuwa na mzaha sana na dharau juu, baadaye wakagundua timu nyingine kama Mbeya City zina ushindani mkubwa”.
“Mwalimu Mecky Mexime amesema atafanyia marekebisho matatizo yote na mzunguko wa pili Mtibwa Sugar itaingia kwa kasi kubwa”. Alisema Kifaru.
Kifaru alisema kutokana na ukongwe wa klabu hiyo, wameamua kukaa chini na kujiandaa vizuri ili kuonesha uzoefu wao mzunguko wa pili”. Aliongeza kifaru.
Afisa habari huyo alitaja timu mbili za Mbeya City FC na Rhino Rangers kuwa bora zaidi na kuleta changamoto kubwa, hivyo wamejiona wana wajibu wa kujipanga kukabiliana na kasi ya vijana hawa ambao ni wapya kabisa.
“Nakuhakikishia kuwa tunatarajia kunoa makucha yetu, tutaingia kwa kasi kubwa mithiri ya Simba au Kifaru aliyejeruhiwa”. Alisisitiza Kifaru.
Mtibwa Sugar wameshiriki ligi kuu kwa miaka takribani 20 na wamewahi kutwaa ubingwa mara mbili mfululizo. Mnamo mwaka wa 1999 na 2000, lakini baada ya hapo wamekuwa wakishika nafasi ya kawaidia sana .
Katika dirisha dogo la usajili hawajaongeza mchezaji yeyote kutokana na mapendekezo ya kocha Mexime aliyewataka kuchana na zoezi hilo kwasababu anao vijana wa kutosha.
Hata hivyo walimpoteza kiungo wao mahiri, Awadh Juma Issa aliyetimkia kwa wekundu wa Msimbazi Simba katika dirisha dogo la usajili.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video