Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini (GEPF) Bwana Daud
Msangi akizungumza na viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Rukwa
alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya kwa
lengo la kuutambulisha mfuko huo na faida zake. Mfuko huo una fursa
mbili za kujiunga ambazo ni kwa njia ya lazima kama ilivyo kwa mifuko
mingine ya hifadhi ya jamii kwa watumishi wa Serikali na njia nyingine
ni ya hiari kwa wafanyakazi wote wakiwemo wa Serikali, Sekta binafsi na
hata wale waliojiajiri wenyewe. Kwa
wale wateja waliojiunga na mfuko huo kwa hiari wana uwezo wa kuchukua
mafao yao kwa muda mfupi tofauti na ule mfumo wa lazima wa Serikali
ambao ni lazima mteja afikie umri wa kustaafu.
Wajumbe
wa kikao hiki walikuwa Wakuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Nkasi na Kalambo.
Wakuu wa Idara wote katika Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa, Wakurugenzi
wa halmashauri za Manispaa ya Sumbawanga, Halmashauri ya Wilaya ya
Sumbwanga, Kalambo na Nkasi pamoja na baadhi ya wataalamu kutoka katika
maeneo hayo.
Mkuu
wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang’a (wa pili kulia) akichangia katika
kikao hicho ambapo alisema Wilaya mpya ya Kalambo ina fursa nyingi za
uwekezaji ikiwemo sekta ya nyumba za ofisi na makazi ambayo ni fursa kwa
mfuko huo wa GEPF kuwekeza kwa kujenga nyumba hizo katika Wilaya hiyo
na Mkoa kwa ujumla. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta. Kulia
kwa Mhe Chang’a ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Albinus Mugonya
na Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Samson
Mashalla.
Sehemu ya wajumbe katika kikao hicho.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)
0 comments:
Post a Comment