Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa Botswana na
Mjumbe wa High Level Group Dr. Festus Mogae wakati wa kikao cha Mawaziri
wa Elimu na Afya kutoka nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika
unaofanyika Cape Town nchini Afrika Kusini tarehe 7.12.2013.
Mawaziri
wa Elimu na Afya kutoka nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wakiapa
kwa niaba ya nchi zao kutekeleza majukumu waliyopitisha kwenye kikao cha
High Level Group, kuhusiana na elimu ya afya ya uzazi ( comprehensive
sexuality education and sexual and reproductive health services)
mwishoni mwa kikao cha siku mbili kilichofanyika huko Cape Town.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha na Mkurugenzi Mtendaji wa
UNAIDS, Bwana Michel Sidibe wakionyesha umuhimu wa dhana nzima ya
mkutano wa High Level Group ( YOUNG PEOPLE TODAY, TIME TO ACT NOW)
kuhusiana na masuala ya elimu ya afya ya uzazi kwa vjijana katika nchi
za Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa Mawaziri kutoka nchi
za Mashariki na Kusini mwa Afrika kuhusu elimu ya afya ya uzazi kwa
vijana wa nchi hizo. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika nchini Afrika
Kusini katika Mji wa Cape Town tarehe 6-7.12.2013.
Baadhi
ya washiriki wa mkutano wakisikiliza hotuba ya ufungaji iliyokuwa
ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete huko Cape Town nchini Afrika
Kusini tarehe 7.12.2013.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na viongozi waandamizi
waliohudhuria mkutano wa High Level Group hukom Cape Town wakisimama kwa
dakika moja kwa ajili ya kumkumbuka hayati Rais Nelson Mandela. Kutoka
kushoto ni Bwana Enver Surty, Waziri wa Elimu ya Msingi wa Afrika
Kusini, Dr. Festus Mogae, Rais Mstaafu wa Botswana, Mama Salma, Bwana
Luiz Loures, Naibu Mkurugenzi Mtendaji, UNAIDS, Dr. Julitha Onabanjo,
Naibu Mkurugenzi Mkuu, UNFPA, Bwana Qian Tang, Naibu Mkurugenzi
Mkuu-Elimu- UNESCO, Bwana Geeta Rao Gupta, Naibu Mkurugenzi Mtendaji,
UNICEF.
PICHA NA JOHN LUKUWI
0 comments:
Post a Comment