Mechi
ya kwanza ya nusu fainali ya michuano ya mwaka huu ya Kombe la Chalenji
kati ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) na wenyeji Kenya (Harambee
Stars) itapigwa Uwanja wa Machakos.
Kwa
mujibu wa ofisa wa CECAFA, Amir Hassan mechi hiyo itachezwa Uwanja wa
Machakos ulioko takribani kilometa 64 kutoka jijini Nairobi. Mechi hiyo
itachezwa Jumanne (Desemba 10 mwaka huu) kuanzia saa 10 kamili jioni na
itaoneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha SuperSport
kupitia chaneli ya SS9.
Kilimanjaro
Stars imetinga hatua hiyo baada ya kuivua ubingwa Uganda (The Cranes)
kwa mikwaju 3-2 ya penalti katika mechi ya robo fainali ya michuano hiyo
iliyochezwa jana Uwanja wa Aga Khan katika Jiji la Mombasa.
Hadi
dakika 90 za kawaida zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana mabao
2-2. Mabao ya Kilimanjaro Stars yalifungwa na Mrisho Ngasa wakati katika
mikwaju ya penalti walofumania nyavu ni Amri Kiemba, Athuman Idd na
nahodha Kelvin Yondani.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment