

Na Denis Mlowe wa Francis Godwin Blogu
MTANGAZAJI wa kipindi cha ‘Mboni Show’ kinachorushwa na luninga ya EATV, Mboni Masimba leo amejumuika pamoja katika hafla na watoto yatima zaidi ya 200 walioko katika mkoa wa Iringa.
Katika hafla hiyo umejumuisha vituo vitatu vya watoto yatima vilivyoko mkoani Iringa vya Upendo center na Tosamaganga na kingine kilichoko katika wilaya ya Mufindi cha Moyo kwa Moyo.
Hafla hiyo ya kula chakula cha mchana na yatima imefanyika katika ukumbi wa Highland hall na kuhudhuriwa na baadhi ya wafanyabiashara maarufu mkoani hapa akiwemo mkurugenzi wa makampuni ya Asas, Salim Abri Asas na mgeni rasmi alikuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi..
Mbali ya kuwalisha watoto hao mboni ametumia muda huwa kuendesha kipindi chake cha Mboni Show kwaa kujumuika na watoto hao.
Watoto yatima hao walipata zawadi mbalimbali ambazo zimetolewa na Mboni.
Mtangazaji huyo amekuwa ni mmoja wa watangazaji wanaojitolewa kwa kiasi kikubwa katika kusaidia watoto yatima na kufikia hatua wakati mwengine kuangusha kilio kutokana na kubanwa na huzuni kutoka kwa watoto hao.
Mboni alisema lengo kuu ni kuwakumbusha watanzania juu ya kuwakumbuka watoto yatima kama ambavyo wamekuwa wakichangia sherehe mbali mbali kama harusi, vipaimara, na kitchen party.
0 comments:
Post a Comment