Saturday, December 14, 2013


Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
Tel: o712461976 au 0764302956
WAKALI wapya wa ligi kuu soka Tanzania bara, `The City Zambarao` au `nyuki wa nyanda za juu kusini`,Klabu ya Mbeya City wapo chimbo maeneo ya Mwakareli Tukuyu jijini Mbeya kujiandaa na ngwe ya lala kwa buriani ya ligi kuu.
Kocha  msaidizi wa klabu hiyo, Maka Mwalwisyi amesema kuwa wanatarajia kuongeza kasi zaidi ya ile ya mzunguko wa kwanza na ndio maana waliingia kambini mapema kujiimarisha.
“Falsafa yetu imejikita zaidi kutumia vijana, tulikaa na wachezaji wetu na kuwaeleza umuhimu wa kubakia klabuni kutokana na mipango mizuri ya kuwafikisha mbali zaidi. Hutujauza mchezaji hata mmoja, wote wapo kambini na wanaendelea kujifua zaidi”. Alisema Maka.
Maka alisema kuna timu kubwa zilishatupia ndoana wakati wa dirisha dogo  la usajili zikitaka kuwanasa vijana wetu, lakini tayari benchi la ufundi lilishawatahadharisha wachezaji kuwa wanaweza kukimbilia fedha na kujiunga na klabu kubwa na wakaishia kukalia benchi kama wenzao waliotangulia.
1aOyaaa fanyeni hivi, sawa?: Kocha mkuu wa Mbeya City FC, Juma Mwambusi (katikati) akiongea na vijana wake, Hassan Mwasapili (kushoto) na Peter Richard (kulia) kwenye moja ya mazoezi yake mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania bara. Picha na Maktaba
“Yuko wapi Said Bahanuz?, yuko wapi Hussein Javu aliyekuwa akitamba na Mtibwa?. Walijiunga na Yanga, mambo yamekuwa magumu kwao, hawapati nafasi. Tumewaeleza vijana wetu kuhusu mazingira hayo  na wanaelewa”. Alisema Maka.
Kocha huyo aliongeza kuwa wanahitaji kuona vijana wao wanafikiria soka la kulipwa ili wapate mafanikio makubwa kama ilivyo kwa Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu  wanaocheza TP Mazembe ya Kongo na kuvuna dola za kutosha.
Aidha Maka alisema watu wengi waliwatabiria kuwa nguvu ya soda, lakini mpaka ngwe ya mwisho ya mzunguko wa kwanza, tayari watu walishaanza kuwaogopa na kuona wana dhamira ya kweli.
“Sasa wanatusikilizia mzunguko wa pili. Sisi tuna wachezaji wengi wa kiwango cha juu, na ndio maana leo hii unaweza kumuona Paul Nonga akicheza, kesho ukamuona Jeremiah John au Mwagane Yeya akicheza nafasi ileile kwa kiwango cha juu. Sasa tunakuja na kasi kubwa na sura mpya yaani tutaongeza mara mbili zaidi”. Alisema Maka.
mbeyaMbeya City ilikuwa timu tishio katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu na kujizolea umaarufu mkubwa miongoni mwa mashabiki ambao waliwafananisha na Tukuyu Stars `Banyambala` ambao enzi zao walipanda ligi kuu na kutwaa taji.
Klabu hiyo inayonolewa na kocha mkuu Juma Mwambusi ilimaliza mzunguko wa kwanza ikiwa na pointi 27 katika nafasi ya tatu sawa na Azam fc waliopo nafasi ya pili wakiwa na pointi 27, huku Bingwa mtetezi Yanga akiwa kileleni na pointi 28.
Nafasi ya nne inakaliwa na watani wa jadi wa Yanga, wekundu wa Msimbazi Simba ambao wameongeza sura mpya kikosini mwao wakiwemo Awadh Issa Juma kutoka Mtibwa, Ivo Mapunda  na Donald Mosoti Omwanwa kutoka Gor Mahia ya Kenya,  Pia yupo Kipa Yaw Berko raia wa Ghana na wengine.
Pia wamebadili benchi la ufundi ambapo aliyekuwa kocha mkuu Alhaj Abdallah Kibaden `King Mputa` na msaidizi wake Jamhuri Kiwhelo `Julio` walifungashiwa virago na nafasi yao kuchukuliwa na kocha raia wa  Croatia, Zdravko Logarusic akisaidiwa na kiungo wa zamani wa klabu hiyo, Seleman Abdallah Matola `Veron`.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video