Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
Tel: 0712461976 au 0764302956
MABINGWA wa ligi kuu soka nchini England, Manchester United wameonywa kuwa mchezaji chaguo la kwanza la kocha David Moyes katika usajili wa dirisha dogo januari mwakani, Marco Reus atawagharimu mpaka pauni milioni 40.
Kiungo Reus ana thamani ya pauni milioni 29.4 ili kumnunua katika mkataba wake katika klabu ya Borussia Dortmund.
Lakini inafahamika kuwa mambo yamebadilika tangu Bayern Munich kuonesha nia ya kumsajili kama walivyofanya kumnunua Mario Gotze majira ya kiangaza ya usajili mwaka huu.


Mabingwa hao wa EPL sasa watatakiwa kuvunja rekodi yao ya usajili ili kumnasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 24.
United wanataka wachezaji wa kiwango cha juu katika nafasi zote kikosini.
Japokuwa sehemu ya kiungo ndio imepewa kiapumbele, pia wako makini kuangalia washambuliaji, beki wa kushoto na beki wa kati kwa mipango ya baadaye kwani Patrice Evra na Rio Ferdinand wanaelekea kumaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu na klabu haitaki kuwaongezea.

Mabingwa hao wa EPL wana pesa za kutosha, walijiandaa kupambana na Real Madrid kujaribu kumsajili Gareth Bale majira ya kiangazi mwaka huu, lakini nyota huyo wa Whales aliamua kwenda Hispania.
Shida kubwa katika dirisha dogo la usajili januari mwakani sio fedha kwa Man United, ukweli ni kwamba wachezaji wengi wanaowataka wapo na timu zao zinazoshiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya, hivyo klabu hizo zinakuwa ngumu kuwaachia wachezaji wao muhimu kikosini.

0 comments:
Post a Comment