Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail, soccerstand na suppersport.com
Tel: 0712461976 au 0764302956
MSHAMBULIAJI Danny Welbeck ametokea benchi na kuipa Manchester United bao muhimu la ushindi dhidi ya Norwich leo hii.
Bao hilo pekee lilifungwa na Webeck katika dakika ya 57 akipokea pasi nzuri kutoka kwa mashambuliaji mwenza, Javier Hernandez maarufu kwa jina la Chicharito.
Man United iliwakosa washambuliaji wake muhimu, Wayne Mark Rooney ambaye hakusafiri na timu kuwafuata Norfolk kutokana na majeruhi. Pia Robin van Persie aliendelea kukosekana, hivyo kipindi chote cha kwanza walikuwa butu mpaka mwokozi Welbeck alipoingia kipindi cha pili.
Katika mchezo mwingine muhimu ulikuwa baina ya Manchester City dhidi ya Crystal Palace katika dimba la Etihad na kushuhudia City wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 na kukalia usukani wa EPL kwa saa wakisubiri matokeo ya mechi ya kesho.
Goooo! Danny Welbeck ametokea benchi na kuipa Manchester United bao la ushindi
Kazi tu!: Mshambuliaji wa United, Welbeck akimlamba chenga mlinda mlango John Ruddy kabla ya kuzamisha mpira nyavuniWamepumua!: Welbeck na wachezaji wenzake wakishangilia bao la ushindi
Baada ya matokeo ya leo, msimamo wa ligi kuu unakuwa kama ifuatavyo, huku mechi za kesho zikisubiriwa;
Pos | Team | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
1 | Manchester City | 19 | 13 | 2 | 4 | 54 | 21 | 33 | 41 |
2 | Arsenal | 18 | 12 | 3 | 3 | 36 | 18 | 18 | 39 |
3 | Chelsea | 18 | 11 | 4 | 3 | 33 | 18 | 15 | 37 |
4 | Liverpool | 18 | 11 | 3 | 4 | 43 | 21 | 22 | 36 |
5 | Everton | 18 | 9 | 7 | 2 | 29 | 17 | 12 | 34 |
6 | Manchester United | 19 | 10 | 4 | 5 | 32 | 22 | 10 | 34 |
7 | Newcastle United | 18 | 10 | 3 | 5 | 29 | 23 | 6 | 33 |
8 | Tottenham Hotspur | 18 | 9 | 4 | 5 | 19 | 24 | -5 | 31 |
9 | Southampton | 18 | 7 | 6 | 5 | 25 | 18 | 7 | 27 |
10 | Hull City | 19 | 6 | 5 | 8 | 22 | 23 | -1 | 23 |
11 | Swansea City | 19 | 5 | 6 | 8 | 24 | 25 | -1 | 21 |
12 | Stoke City | 18 | 5 | 6 | 7 | 18 | 26 | -8 | 21 |
13 | Aston Villa | 19 | 5 | 5 | 9 | 18 | 25 | -7 | 20 |
14 | Norwich City | 19 | 5 | 4 | 10 | 16 | 32 | -16 | 19 |
15 | West Bromwich Albion | 19 | 3 | 9 | 7 | 22 | 27 | -5 | 18 |
16 | Cardiff City | 19 | 4 | 6 | 9 | 15 | 30 | -15 | 18 |
17 | Crystal Palace | 19 | 5 | 1 | 13 | 12 | 28 | -16 | 16 |
18 | Fulham | 19 | 5 | 1 | 13 | 19 | 41 | -22 | 16 |
19 | West Ham United | 19 | 3 | 6 | 10 | 18 | 28 | -10 | 15 |
20 | Sunderland | 19 | 3 | 5 | 11 | 15 | 32 | -17 | 14 |
Bao la ushindi lililowafanya Manchester City wabarizi kileleni kwa saa lilifungwa na Edin Dzeko dakika 66 akipokea pasi kutoka kwa Jesus Navas.
Kazi rahisi tu: Mshambuliaji wa Manchester City, Edin Dzeko akifunga bao la ushindi dhidi ya Crystal Palace
Dzeko (kulia) akishangilia bao lake, huku wachezaji wa Palace wakiduwaa
Tumepumua jamani!: Dzeko akipongezwa na Alvaro Negredo (kushoto) baada ya kuvunja ngome ngumu leo hii katika dimba la Etihad
MATOKEO YA MECHI ZA LEO NI KAMA IFUATAVYO;
Finished
|
West Ham
| 3-3 |
West Bromwich Albion
| (1-2) | ||||||
Finished
|
Aston Villa
| 1-1 |
Swansea
| (1-1) | ||||||
Finished
|
Hull
| 6-0 |
Fulham
| (0-0) | ||||||
Finished
|
Norwich
| 0-1 |
Manchester United
| (0-0) | ||||||
Finished
|
Manchester City
| 1-0 |
Crystal Palace
| (0-0) | ||||||
Finished
|
Cardiff
| 2-2 |
Sunderland
|
Manchester City wamefikisha pointi 41 kileleni, lakini yawezekana wamekaa kwa saa kadhaa kwani Arsenal ambao wapo nafasi ya pili na pointi 39 watacheza kesho dhidi ya Newcastle United.
RATIBA NI KAMA YA MECHI ZA KESHO NI IFUATAVYO;
29/12 16:30
|
Newcastle United
| - |
Arsenal
| ||||||
29/12 16:30
|
Everton
| - |
Southampton
| ||||||
29/12 19:00
|
Tottenham
| - |
Stoke
| ||||||
29/12 19:00
|
Chelsea
| - |
Liverpool
|
0 comments:
Post a Comment