………………………………………………………………
Wakati
Nelson Mandela anaongoza Afrika Kusini dhidi ya ubaguzi wa rangi na
baadaye kuwa kiongozi maarufu duniani baada ya kutoka jela, inabidi
tujiulize ni watu gani ambao walikuwa karibu naye kifamilia, kiroho na
kuumia naye na waliomfahamu zaidi ya wote?
Baba
yake Mandela alimwacha akiwa na miaka tisa baada ya kufariki mwaka
1927, baadaye alilelewa na Chifu Jongintaba kabla ya kutoroka baada ya
kutaka kuozwa akiwa bado mdogo.
Wakati
anaanzisha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi na kupigania usawa,
ilikuwa dhahiri Mandela alihitaji kuwa na mwanamke mkakamavu na jasiri.
Mandela
ameishi na wake watatu katika maisha yake – EvelynMase, Winnie
Madikizela na wa mwisho, Graca Machel alimuoa akiwa anatimiza miaka 80.
Mandela
amekuwa kipenzi kwa watoto na masuala ya elimu na kwa kudhihirisha hilo
aliaanzisha Mfuko maalumu wa elimu kwa ajili ya watoto, ukiwa ni sehemu
ya mafanikio katika maisha yake.
Nelson
Mandela ni baba wa watoto sita, wanne akiwazaa kwenye ndoa ya kwanza na
Evelynna wengine wawili kwa mkewe wa pili, Winnie.
Watoto
wa Mandela wamepitia katika kipindi kigumu na wana kitu cha kipekee
katika maisha yao, kwani kuna wengine ambao hawakupata kuonana na baba
yao maisha yao yote, kwani alikuwa jela katika kipindi cha uhai wao.
Mabinti
wa Mandela waliozaliwa kwa mke wa kwanza waliitwa Makazawie. Mkubwa
alikufa miezi tisa baada ya kuzaliwa na mwingine aliyemfuata ilibidi
apewe heshima ya jina hilo kwa ajili ya dada yake.
Mwingine,
Madiba Thembikile (Thembi) alikufa kwa ajali ya gari mwaka 1969 akiwa
na miaka 25. Mandela alikuwa jela kipindi hicho na hakuruhusiwa
kuhudhuria mazishi ya mwanawe.
Makgatho alikufa mwaka 2005 baada ya kuugua ugonjwa wa Ukimwi.
Ndio
maana Nelson Mandela amekuwa mwanaharakati mkubwa wa mapambano dhidi ya
ugonjwa huo na alianzisha kampeni dhidi ya ugonjwa huo aliyoiita 46664
AIDS Campaign, jina likitokana na namba yake akiwa jela.
Mandela na Evelyn walidumu katika ndoa kwa miaka 13 na kuachana mwaka 1957.
Waliachana
kwa sababu mwanamke huyo alikuwa Shahidi wa Yehova na imani yao
iliwataka wasishabikie masuala ya siasa. Mwanamke huyo alifariki dunia
mwaka 2004.
Mwaka 1958 Mandela alimuoa Winnie Madikizela. Ingawa sehemu kubwa ya muda wa ndoa yao aliutumia akiwa jela.
Winnie alikuwa mwanamke shupavu kwani naye alikuwa mwanasiasa machachari.
Walifanikiwa kuzaa mabinti wawili Zenani (Zeni) –aliyezaliwa mwaka 1958, na Zindziswa (Zindzi) – aliyezaliwa 1960.
Zeni
aliolewa na mtoto wa mfalme, Prince Thumbumuzi Dlamini. Zindzi
alijiandikia historia mwaka 1985 pale alipotoa hotuba ya kupinga baba
yake kutolewa jela kwa masharti.
Kutokana na tofauti za kisiasa na za kibinafsi, Mandela na Winnie walilazimika kuachana mwaka 1994.
Mwaka
1988 alipotimiza miaka 80 ya kuzaliwa, Mandela alimuoa Graca Machel
(Mjane wa Rais wa Msumbiji, Marehemu Samora Machel ambaye aliyekufa
kwenye ajali ya ndege inayodhaniwa ilitunguliwa na Makaburu mwaka 1989.
Nelson
Mandela alikuwa akiishi katika nyumba yake iliyoko Qunu. Pamoja na
kwamba ana nyumba nyingi sehemu mbalimbali duniani, lakini sehemu
aliyoipenda ni kijijini kwao katika jimbo la Transkei.
CHANZO: MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment