Saturday, December 14, 2013

gurumo poster
HATIMAYE ile siku iliyokuwa inasubiriwa na wengi, imewadia, ni GURUMO 53 ndani ya viwanja vya TCC Club, Chang’ombe leo Jumamosi Disemba 14.
Kama tangazo linavyojionyesha, ni tamasha kubwa la muziki wa dansi la kustaafu kwa gwiji Muhidin Maalim Gurumo aliyeitumikia fani hiyo kwa miaka 53 mfululizo.
Gurumo ataimba angalau wimbo mmoja au zaidi wa kila bendi aliyopitia katika safari yake ndefu kimuziki.
Hadi kustaafu kwake Gurumo aliyezitumikia pia bendi za Kilimanjaro Chacha, Rufiji Jazz, Kilwa Jazz, Sikinde na OSS – Ndekule, alikuwa ni kiongozi na mmoja wa wamiliki wa Msondo Ngoma ambayo hapo awali ilijulikana kwa majina ya NUTTA, Juwata na OTTU. Gurumo ameitumika Msondo katika majina yote ya nyuma.
Ama kwa hakika ni burudani ya kukata na shoka, bendi kibao, wasanii kibao – ni burudani mwanzo mwisho kuanzia saa 12 jioni mpaka majogoo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video