Monday, December 9, 2013

Picha na 1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi alipokua akiwasili uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange.
Picha na 2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akipokea salam ya Rais na kupigiwa mizinga 21 kutoka kwa gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi ya Tanzania leo uwanja wa Uhuru mara baada ya kuwasili.
Picha na 3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi na usalama leo uwanja wa Uhuru wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.Picha na 4Sehemu ya askari wa vikosi vya ulinzi na usalama wakiwa wamesimama kwa ukakamavu wakati kabla ya kamanda wa gwaride kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kukagua gwaride hilo leo jijini Dar es salaam.Picha na 5Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete  akiwasili jukwaa kuu la Uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo.Picha na 6 Gwaride likipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa mwendo wa haraka.Picha na 7Rais Jakaya Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange wakati gwaride la vikosi vya Ulinzi na Usalama likipita mbele ya jukwaa kuu  la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa haraka.Picha na 8Baadhi ya Maofisa wa jeshi wakipiga saluti wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.
Picha na 9Wananchi wa mkoa wa Dar es salaam waliojitokeza kuhudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es salaam.Picha na 10Vijana wa halaiki kutoka Tanzania Bara na Visiwani wakitamka kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo jijini Dar es salaam ambayo ni “ Vijana ni Nguzo ya Rasilimali Watu,Tuwaamini, Tuwawezeshe na Tuwatumie kwa Manufaa ta Taifa Letu”Picha na 11Vijana wa halaiki wakiendelea kuwasilisha jumbe mbalimbali kama inavyoonekana mfano wa mnyama aina ya samba kuashiria utalii katika hifadhi  za wanyama za Tanzania.
Picha na 12Vijana wa halaiki wakionyesha ukakamavu.Picha na 14Ujumbe ukiwasilishwa kwa njia ya picha kuhusu viongozi wapigania Uhuru wa Tanzania Bara, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Picha na 15Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akitoa hatuba fupi kwa watanzania wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Hatuba yake licha ya kujaa maneno ya kumkumbuka rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini  Mzee Nelson Rolihlahla Mandela Madiba  aliyeaga dunia juzi nchini Afrika ya Kusini imesisitiza Upendo, Amani, Mshikamano miongoni mwa  watanzania na kukemea tabia ya baadhi ya viongozi kulipiza kisasi pindi waingiapo madarakani.Picha na 16Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein (kushoto), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange wakisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo katika uwanja wa Uhuru wakati wa Maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.Picha na 17Raia wa kigeni waliohudhuria sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara wakisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo.Picha na 18Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange alipokua akisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo.Picha na 19Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelo Freeman Mbowe akiwa miongoni mwa viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video