Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akizungumza na waandishi wa habari leo
jijini Dar es salaam kuhusu kukamilika kwa maadalizi ya sherehe za
miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara zitakazofanyika tarehe 9 Desemba
katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam
Vikosi
vya majeshi ya Ulinzi na Usalama vya Tanzania vikiendelea na maadalizi
ya maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru na gwaride maalum leo jijini Dar es
salaam.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Na Aron Msigwa –MAELEZO, Dar es salaam.
Zikiwa
zimebaki siku mbili Tanzania iadhimishe miaka 52 ya Uhuru, Mkuu wa Mkoa
wa Dar es salaam Saidi Meck Sadick ametoa wito kwa watanzania
kusherehekea maadhimisho hayo kwa kuenzi , kulinda na kudumisha
mafanikio makubwa yaliyopatikana tangu Uhuru.
Akizungumza
na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam Meck Sadiki amesema kuwa
Tanzania katika kipindi cha miaka 52 ya Uhuru imepata mafanikio makubwa
ya kiuchumi, ulinzi, usalama pamoja na uhusiano wa kimataifa na kuongeza
kuwa mafanikio hayo yanatokana na umoja na mshikamano ulioonyesha tangu
kuasisiwa kwa taifa la Tanzania.
“Kipindi
chote cha miaka 52 ya Uhuru tumepata mafanikio makubwa sana na ya
kujivunia kiuchumi, ulinzi na usalama pamoja na uhusiano wa kimataifa,
tuna kila sababu ya kuendeleza mafanikio haya”
Amesema
maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru kwa mwaka 2013 kitaifa yatafanyika
katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na kuongozwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete chini ya kauli mbiu
isemayo “Vijana ni Nguzo ya Rasilimali Watu, Tuwaamini, Tuwawezeshe na
Tuwatumie kwa Manufaa ya Taifa Letu”
Ameongeza
kuwa maadhimisho ya mwaka huu yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa
ndani na nje ya nchi na kupambwa na burudani za vikundi vya ngoma za
asili kutoka bara na visiwani,Gwaride maalum la vikosi vya ulinzi na
Usalama, kwaya mbalimbali, bendi za muziki, maonyesho ya ndege za
kijeshi na halaiki maalum.
Ametoa
wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi na kuwahi mapema wakati wa
maadhimisho hayo na kubainisha kuwa kutokana na maadalizi mazuri
yaliyofanyika milango ya uwanja wa Uhuru itakuwa wazi kuanzia saa 12:30
Asubuhi.
0 comments:
Post a Comment