Saturday, December 14, 2013

lowassa+clipAbiria 37 waliokuwa wamesafaria ndege ya Shirika la Precision Air, akiwamo Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, jana walinusurika kifo, baada ya magurudumu manne ya ndege hiyo kupasuka ilipokuwa ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Arusha. 
………………………………………………………………………..
Arusha. Abiria 37 waliokuwa wamesafaria ndege ya Shirika la Precision Air, akiwamo Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, jana walinusurika kifo, baada ya magurudumu manne ya ndege hiyo kupasuka ilipokuwa ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Arusha.
Tukio hilo la aina yake, lilitokea saa 6:15 mchana, wakati ndege hiyo, ikitua kutoka jijini Dar es Saalam, ikiwa na abiria hao 37, marubani wawili na wahudumu wawili.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza hakuna majeruhi aliyeripotiwa.
“Hadi sasa hali ni shwari, ndege iliweza kusimama licha ya kupasuka magurudumu. Kiutaratibu uchunguzi umeanza kufanywa na wataalamu husika,”alisema Kamanda Sabas.
Ofisa Mwendeshaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TCAA), wa Uwanja wa Ndege Arusha, Roland Mwalyambi, alisema kuwa katika tukio hilo, hakuna abiria aliyejeruhiwa licha ya kupata mshtuko mkubwa.
“Uchunguzi wa ajali hii umeanza, lakini hakuna majeruhi, abiria wote walifanikiwa kushuka salama,”alisema Mwalyambi.
Alisema ndege hiyo, kama ingetua salama ilitarajiwa kusafiri kurejea Dar es Salaam kupitia Zanzibar, lakini abiria waliotarajia kusafiria ndege hiyo, walipelekwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro ili kuendelea na safari.
Katika ndege hiyo, pia kulikuwa na maofisa mbalimbali wa Serikali na Jeshi la Wananchi, ambao leo wanatarajia kuhudhuria sherehe ya kutolewa kamisheni kwa maofisa wa jeshi katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli(TMA), ambapo Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Tukio hilo la ndege kupata ajali katika uwanja huo ni la pili kutokea mwaka huu, kwani mapema mwaka huu, mfanyabiashara maarufu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha, Babu Sambeki alipata ajali pia katika uwanja huo, wakati akijiandaa kutua na ndege yake.
Mfanyabiashara huyo, alifariki papo hapo baada ya moja ya mabawa ya ndege kunasa katika matawi ya mti jirani na uwanja huo. Hata hivyo, taarifa ya ajali hiyo hadi sasa haijawekwa hadharani.
Kukosekana kwa taa katika uwanja huo, ambao umekuwa ukitumiwa na ndege nyingi ndogo hasa za watalii, imekuwa ni kero kubwa na mara kadhaa safari zimeahirishwa kutokana na tatizo hilo.
CHANZO: MWANANCHI

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video