Kocha mpya wa Simba SC (wa pili kulia), Mcroatia, Zdravko Logarusic, ataiongoza klabu hiyo kwa mara ya kwanza katika mechi ya kirafiki dhidi ya KMKM katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam leo jioni, ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa kuhitimisha kampeni ya NANI MTANI JEMBE?, mnamo desemaba 21 mwaka huu dhidi ya watani wao wa jadi, Dar Young Africans.
…………………………………………………………………….
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
Tel: 0712461976 au 0764302956
WEKUNDU wa Msimbazi , Simba SC leo wanashuka katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam kugegeduana na KMKM kutoka Zanzibar katika mchezo wa kirafiki.
KMK wanaingia katika mchezo wa leo wakiwa na machungu ya kupigwa mabao 3-2 hapo jana na mabingwa watetezi na vinara wa ligi kuu soka Tanzania bara, Dar Young Africans.
Mabao ya Yanga yalifungwa na Jerryson John Tegete, Nadir Haroub `Canavaro na Khamis Thabiti, huku KMKM mabao yake yakifungwa na Hajji Simba na Ally Ahmed “Shiboli`.
Mchezo wa leo ni muhimu kwa Simba kupima uwezo wa kikosi chake kabla ya kukutana na watani wake wa jadi, Yanga, katika mchezo maalumu wa kuhitimisha kampeni ya `NANI MTANI JEMBE?`, desemba 21, uwanja wa Taifa.
Simba itaingia na sura mpya ya benchi la ufundi ambapo kocha wake mkuu, Mcroatia Zdravko Logarusic akisaidiwa na Seleman Abdallah Matola watakalia benchi kuona kikosi chao walichopokea kutoka kwa Abdallah Kibadeni na Jamhuri Kiwhelo `Julio` waliotimuliwa kwa madai ya kupata matokeo mabaya.
Mbali na benchi la ufundi kuwa jipya, pia wapo wachezaji wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo la usajili.
Miongoni mwa wachezaji wapya wa Simba Sc ni kiungo Juma Awadh Issa kutoka Mtibwa sugar, kipa Ivo Mapunda na beki Donald Mosoti Omwanwa wote kutoka Gor Mahia ya Kenya, Yaw Berko raia wa Ghana na wengine.
Mashabiki wa Simba wanaingia uwanjani leo hii kuona kiwango cha klabu hiyo baada ya mabadiliko hayo na kutathimini kama wataweza kuwatungua Yanga mechi ijayo.
Mara ya mwisho Simba na Yanga kukutana ilikuwa Octoba 20 mwaka huu katika kipute cha ligi kuu ambapo timu hizo zilitoka sare ya 3-3 , uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Yanga walianza kufungwa mabao 3-0 katika dakiza 45 za kwanza, Simba SC wakachomoa zote kipindi cha pili.
0 comments:
Post a Comment