MSHAMBULIAJI wa Liverpool , Luis Suarez ameongeza presha zaidi kwa kocha Andre Villas-Boas baada ya kufunga mabao mawili katika ushinidi 5-0 dhidi ya Tottenham .
Mabao ya Liverpool leo hii yamefungwa na Suarez dakika ya 18, Henderson dakika ya 40, Flanagan dakika ya 75, Suarez tena katika dakika ya 84, na Sterling alihitimisha karamu ya maboa dakika 89.
Suarez aliyevishwa kitambaa cha unahodha alifanya kazi kubwa katika ushinid huo na kuwafanya mashabiki wa Tottenham wawe na presha kubwa na wengi wao waliondoka mapema na kuwaacha wenzao wachache wakikaa hadi dakika za mwisho.
Safu ya ulinzi ya Spurs ilionekana kuwa dhaifu zaidi mbele ya washambuliaji wa Liverpool na matokeo ya leo yanamuweka kitimoto kocha Villas-Boas, hasa baada ya kupoteza mchezo mwingine kwa kipigo cha mbwa mwizi kutoka kwa wapinzania wao Manchester City wiki chache zilizobaki.
Jembe: Luis Suarez, nahodha wa leo akishangilia bao lake baada ya Liverpool kuanza vyema katika mchezo wa leo
MSIMAMO
Team P GD Pts 1 Arsenal 16 16 35 2 Liverpool 16 21 33 3 Chelsea 16 14 33 4 Manchester City 16 29 32 5 Everton 16 12 31 6 Newcastle United 16 -1 27 7 Tottenham Hotspur 16 -6 27 8 Manchester United 16 6 25 9 Southampton 16 5 24 10 Swansea City 16 1 20 11 Aston Villa 16 -5 19 12 Hull City 16 -6 19 13 Stoke City 16 -5 18 14 Norwich City 16 -14 18 15 Cardiff City 16 -10 17 16 West Bromwich Albion 16 -5 15 17 West Ham United 16 -6 14 18 Crystal Palace 16 -13 13 19 Fulham 16 -15 13 20 Sunderland 16 -18 9
MATOKEO YA MECHI ZA JANA
England: Premier League
Finished
|
Aston Villa
| 0-3 |
Manchester United
| (0-2) | |||||
Finished
|
Norwich
| 1-1 |
Swansea
| (1-1) | |||||
Finished
|
Tottenham
| 0-5 |
Liverpool
|
0 comments:
Post a Comment