Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kwenye treni huku akilakiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Madabida katika kituo kikuu cha reli ya TAZARA leo asubuhi jijini Dar es salaam wakati alipowasili akitoka kwenye ziara yake ya kikazi ya mikoa mitatu ya Ruvuma, Mbeya na Njombe akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa na mbunge wa kuteuliwa pamja na jopo la waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliokuwa katika ziara hiyo.(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akissalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhan Madabida, wanaoshuka kwenye treni ni Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa na mbunge wa kuteuliwa na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi mara baada ya kuwasili na treni ya TAZARA leo asubuhi.Abdulrahmani Kinana akivishwa skafu na vijana wa CCMAkeielekea eneo lililoandaliwa kwa mapokeziMwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Madabida akielezea machache juu ya mafanikio ya ziara hiyo.Kinana akisalimiana na wana CCM mbalimbali waliofika kumpokea kituo kikuu cha TAZARA.Kinana akizungumza na wana CCM waliokuja kumpokea yeye na msafara wake na kuwashukuru.Nape Nnauye akitoa shukurani zake kwa waandishi wa habari na vyombo mbalimbali vilivyofanya kazi ya kutangaza ziara hiyo kushoto ni Ndugu Abdulrahman Kinana Katibu Mkuu wa CCM.Kinana akiwa amejichanganya na wananchi katika kituo cha treni la TAZARA cha Mlimba mkoani Morogoro jana akiwa njiani kurejea Dar es salaam.Wanahabari waliokuwa kwenye msafara wa katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman kinana wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kuwasili jijini Dar es salaam leo asubuhi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Dr. Asha Rose Migiro katikati na Nape Nnauye wakishuka kwenye treni mara baada ya kusimama kwa muda katika kituo cha Mlimba mkoani Morogoro kwa ajili ya kuzungumza kidogo na wananchi.Abdulrahman kinana akilakiwa na viongozi wa CCM kata ya Mlimba Abdulrahman Kinana akinawa mikoni kituoni hapoKinana na ujumbe wake wakielekea katika jengo la abiria kituoni hapoHapa akizungumza na mmoja wa wachuuzi wa samaki kituoni hapo.Nape nnauye akichagua samaki, kulia anayeangalia ni Dr. Asha Rose MigiroKatibu Mkuu wa CCM Abdulrahman kinana akizungumza na mkuu wa kituo cha Polisi TAZARA Mlimba ACP Boniface Haule wakati alipofika kituoni hapo na kuongea na wasafiri mbalimbali akisafuiri na treni hiyo kuelekea Dar es salaam. Kinana akijichanganya na wananchi katika kituo cha Mlimba Mkoani Morogoro.
0 comments:
Post a Comment