Mbozi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Dk Charles
Mkambachepa juzi alionja joto la jiwe baada ya Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahaman Kinana kumtaka arudishe haraka Sh209 milioni za Saccos ya
Chama cha Walimu zilizochukuliwa na halmashauri hiyo katika mazingira ya
kutatanisha kuanzia Mei mwaka huu.
Hali
hiyo ilijitokeza juzi jioni wakati Kinana alipozungumza na baadhi ya
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi hususan walimu.
Dk
Mkambachepa alilazimika kutamka wazi kwamba atahakikisha anawalipa
fedha zote ifikapo mwishoni mwa Januari mwaka ujao na kwamba juzi hiyo
aliwalipa zaidi ya Sh32 milioni kupunguza deni hilo.
Awali
Kinana alipokea taarifa ya malalamiko lukuki ya walimu yakiwamo ya
madai ya zaidi ya Sh1 bilioni na pia halmashauri kuchukua Sh209 milioni
za makato ya walimu kwa ajili ya kurudisha mikopo ya Saccos.
Walimu
walidai halmashauri hiyo chini ya Mkurugenzi mstaafu Edson Chelewa
ilichukua fedha hizo ikidai zinatumika katika masuala ya kumpokea Rais
Jakaya Kikwete kwenye sherehe za Mei Mosi zilizofanyika kitaifa mkoani
Mbeya.
Kutokana
na kauli hiyo, Katibu Mkuu wa CCM alisema huo ni uzushi wa hali ya juu
na kuitaka halmashauri hiyo kuacha mara moja tabia ya kuwaonea walimu
kwa kusingizia viongozi mambo mabaya ya fitina.
“Kuanzia
sasa CCM imeamua kuingia kati kufuatilia matatizo ya walimu yakiwamo
madai yao na kwa kweli itahakikisha yanalipwa” alisema.
Awali
akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Baraza la Kata, Kinana
aliwasihi Watanzania kuendelea kuiamini Serikali ya CCM akisisitiza
inalenga kuwatetea wanyonge na kuboresha maisha.
CHANZO: MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment