Na Baraka Mpenja
Tel: 0712461976
KOMBE
la Mataifa ya Afrika mashariki na kati , CECAFA Challenge 2013
limefikia patamu zaidi kwa mechi za kwanza za Robo fainali kupigwa leo
hii Uwanja wa Manispaa, Mombasa, Kenya.
Mechi
inayosubiriwa kwa hamu na kuvuta hisia za mashabiki wengi wa kandanda
ni baina ya mabingwa watetezi, Korongo wa Kampala, Uganda The Cranes
dhidi ya Nyota wa Kilimanjaro, timu ya Taifa ya Tanzania bara, The
Kilimanjaro stars itakayoanza majira ya saa 8:00 mchana, ingawa kutakuwa
na mech nyingine ya kukata na shoka kati ya wenyeji , Kenya dhidi ya
Amavubi, Timu ya Taifa ya Rwanda majira ya saa 10:00 jioni.
Hata
hivyo Kili Stars wanaingia uwanjani leo wakiwa na kumbukumbu mbaya na
unyonge wa kufungwa kwa mfululizo na Uganda katika mechi za hivi
katibuni.
Uganda
inayonolewa na kocha mahiri na aliyewahi kufanya kazi na Yanga ya Dar
es salaam, timu ya Taifa ya Rwanda na maeneo mengine Afrika , Mserbia
Milutin Sredojevic ‘Micho’ itaingia uwanjani na nguvu na ujasiri zaidi
kutokana na matokeo mazuri ambayo imekuwa ikipata siku za karibuni dhidi
ya stars.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Kilimajaro Stars leo hii
Taifa
stars ambayo kwa kiasi kikubwa inaundwa na wachezaji wa Kilimanjaro
stars katika mechi mechi mbili za karibuni za kuwania kucheza fainali za
mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani, CHAN, ilifungwa nyumbani na
ugenini na The Cranes.
Ilikula 1-0 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, ikaenda kumalizwa jijini Kampala uwanja wa Nelson Mandele Namboole mabao 3-1.
Katika
michuano ya CECAFA mwaka jana mjini Kampala nchini Uganda, Kili stars
ilivaana na Uganda katika mchezo wa nusu fainali na kula kisago kama
kawaida cha mabao 3-0.
Katika
mchezo wa mwaka jana, Uganda walikuwa tishio kubwa zaidi kutokana na
uwezo mkubwa wa wachezaji wao wakiwemo Emmanuel Okwi na Khamis Kiiza.,
hivyo waliwazidi Stars kwa kila kitu uwanjani.
Mwaka
huu, Stars imetinga robo fainali kwa kushindi mechi mbili dhidi yya
Somali 1-0, Burundi 1-0 na sare ya bao 1-1 na waliowahi kuwa mabingwa wa
Afrika, timu ya Taifa ya Zambia `Chipolopolo` na kushika nafasi ya
pili ya Kundi B.
Kwa
upande wa Uganda, ni balaa tupu, wametinga robo fainali kwa kushinda
mechi zote za kundi C wataalamu wengi wa soka wanapenda kuita ushindi wa
asilimia mia moja,
Mchawi!:
Emmanuel Anord Okwi ni miongoni mwa Waganda wenye akili kubwa ya mpira,
huwa ni hatari sana na ukicheza naye vibaya unavuna mabua
Wakati
homa ya pambano ikizidi kupanda, makocha wa timu zote tayari
wameshamwaga sera zao huku kila mmoja akiongea kwa tahadhari kubwa
zaidi.
Koha
wa Kili Stars Mdenmark, Kim Paulsen ameseme mechi ni ngumu na
anawaheshimu sana Uganda kwani ni timu nzuri yenye wachezaji wakali,
lakini amejiandaa kupambana kufa na kupona katika mchezo wa leo.
Micho
kwa upande wake amekiri ubora wa Stars hasa baada ya kuwasili kwa
Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaocheza TP Mazembe ya DRC Kongo,
lakini akiwemo pia Mjomba Mrisho Khalfan Ngassa.
Ukiangalia
maneno ya makocha wote wawili, kwa haraka haraka utagundua kuwa
wanaogopana sana kuelekea mchezo huu na hii inadhihirisha mchezo utakuwa
mgumu sana.
Safu
ya ushambuliaji ya Stars leo inatarajiwa kuongozwa na Mrisho Ngassa,
Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta wakati viungo wanaweza kuwa Frank
Domayo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Athumani Iddi ‘Chuji’.
Thomas Ulimwengu ana machungu sana na Waganda leo, anatamani muda ufike akawaoneshe kazi kama afanyavyo huko TP Mazembe
Langoni
ataanza Mkongwe Ivo Philp Mapunda, kulia Himid Mao, kushoto Erasto
Nyoni na katikati Said Morad na Kevin Patrick Philip Yondan.
Kwa
upande wa mabingwa watetezi, Uganda, Emanuel Anord Okwi, Hamisi Friday
Kiiza na Dani Sserunkuma wanatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji,
wakati wengine kikosini watakuwa Nico Wadada, Godfrey Kizito, Khalid
Aucho, Brian Majwega, Vincent Kayizzi, Godfrey Walusimbi, Savio Kabugo
na Benjamin Ochan langoni.
Fundi wa Jangwani!: Khamis Friday Kiiza ni hatari tupu ukimwachia
Robo fainali za pili zitapigwa kesho ambapo Zambia wakatakabiliana na Burundi, huku Ethiopia wakioneshana kazi na Sudan.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Kilimanjaro Stars.
0 comments:
Post a Comment