Sunday, December 15, 2013

Wakiwa-katika-picha-ya-pamoja-meneja-wa-kinywaji-cha-Guinness-Davis-Kambikatikati-na-washiriki-wa-Guinness-Football-Challenge-baada-ya-kupokea-hati-zao-za-kusafiria.Na Gladness Mushi, Arusha
KIKUNDI cha Olgilai Changamkeni Youth Group kilichopo maeneo ya Olgilai mkoani Arusha kwa kushirikiana na wadau wengine wa elimu wameweza kutoa msaada wa madawati zaidi ya 54 yenye thamani ya zaidi ya Milioni tatu na nusu  pamoja na vifaa vingine kama vile meza, kabati, na viti  kwa shule ya msingi Olgilai huku lengo likiwa ni punguza changamoto za kielimu shuleni hapo hasa changamoto ya kukaa chini kwa wanafunzi.
Hataivyo msaada huo ambao ulitolewa mapema jana ulienda sanjari na uzinduzi wa kikundi hicho ambacho kimelenga kutatua changamoto mbalimbali katika kijiji hicho cha Olgilai na Mkoa wa Arusha kwa ujumla.
Akiongea mara baada ya kukabidhi msaada huo kwa shule ya msingo Olgilai Mwenyekiti wa kikundi hicho Benjamini Justin alisema kuwa wameamua kuchangia zoezi zima la elimu ili kwenda sanjari na mpango wa serikali wa matokeo ya haraka(BRN)
Benjamini alidai kuwa hapo awali shule hiyo ilikuwa inakabiliwa na changamoto kubwa sana ya ukosefu wa madawati na vifaa vingine hali ambayo ilifanya wazazi wa eneo hilo ambao ni wanakikundi kuhakikisha kuwa wanatafuta mbinu ya kukabiliana na changamoto hiyo.
Alifafanua kuwa baada ya kuweka mikakati mbalimbali waliweza kuwashirikisha wadau wengine ambao nao waliweza kuungamkono na kuhakikisha kuwa wanapunguza tatizo la uhaba wa madawati kwenye shule hiyo ya Olgilai.
Wakati huo huo alidai kuwa pamoja na kuwa wameweza kufanikisha kutoa msaada huo wa madawati, meza,viti, madaftari, na kalamu lakini bado wanakabiliwa na changamoto lukuki ambazo wakati mwingine zinakwamisha jitiada zao
Alitaja changamoto hiyo kuwa ni pamoja na baadhi ya fursa za mikopo ni finyu kwa kuwa taasisi hizo hazitoi mikopo kwa vikundi jambo ambalo linakwamisha jitiada za maendeleo ya vikundi hasa vile vya mitaa.
Wakati huo huo akiongea kwa niaba ya wanafunzi ambao ndio walengwa wa msaada huo Irene Peter alidai kuwa msaada huo wa madawati utasaidia sana kuongeza ufanisi wa elimu kwani hapo awali wanafunzi shuleni hapo walikuwa wanalazimika kuandika Miandiko mibaya kwa kuwa hawakuwa na madawati.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video