Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akizungumza katika mahafali ya kwanza ya shule ya Awali ya Istiqaama iliyopo Majumbasita katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa Katika hotuba yake hiyo aliwaasa waislamu kuwaendeleza watoto wao kielimu katika taasisi za kidini zilizopo ili waweze kupata elimu zote za kitaaluma na kidini waweze kuwa na ujuzi na maadili mema. Aliwataka pia Waislamu kujenga tabia ya kuchangia taasisi zao ili ziweze kusonga mbele katika malengo waliojiwekea. Pichani kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Adam Misana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Istiqaama English Medium and Primary School ya Sumbawanga Amr Said akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza katika mahafali hayo. Katika risala iliyosomwa kwa Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima Shule hiyo ilianza rasmi Januari mwaka huu 2013 ikiwa na wanafunzi 48 na hidi hivi sasa ina wanafunzi 6. Shule hiyo inayoendeshwa na taasisi ya kidini ya ISTIQAAMA ina mpango wa kujenga shule ya msingi katika kipindi cha mwaka 2014-2017 na shule ya Sekondari katika kipindi cha mwaka 2018-2021.
Baadhi ya watoto wakiwa wanacheza katika moja ya sehemu za michezo katika shule hiyo. Pichani nyuma ni sehemu ya madarasa ya shule hiyo.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)
0 comments:
Post a Comment